Askofu
mkuu wa kanisa la waadventista wasabato jimbo kuu la Afrika Mashariki na
Kati Mchungaji Dkt. Blasious Ruguri
Askofu
mkuu wa kanisa la waadventista wasabato jimbo kuu la Afrika Mashariki na
Kati Mchungaji Dkt. Blasious Ruguri amesema serikali ya Tanzania ya awamu ya
tano imepata mafanikio makubwa ya ungozi ya kukuza uchumi katika kanda ya
afrika mashariki kiasi cha kuwafanya wananchi wa nchi jirani kuwataka viongozi
wao wakajifunfu kwa Rais Dkt. John Magufuli.
Pia
Dkt. Ruguri amesema nchi ya Tanzania ni mfano wa kuigwa na nchi za afrika kwa
kuwa imekuwa kinara wa kulinda amani jambo ambalo linaifanya iwe nchi ya namna
yake Afrika kutokana na kuwepo kwa amani ya kutosha nchini.
“Hakuna
matatizo makubwa yanayoripotiwa kwenye vyomba vya kimataifa kama ilivyo nchi
zingine, yanayotokea ni yale madogo madogo ambayo yana malizwa ndani, wananchi
muungeni mkono rais wetu Magufuli kwa kuwa anamcha Mungu jambo ambalo ni zuri
kwa kiongozi wan chi kumtanguliza Mungu katika shughuli zake hakika atafanikiwa
maana viongozi wote wamewekwa na Mungu na pale wanapo acha kumtegemea naye
huwaacha na kuharibikiwa katika uongozi wao,” alisema Askofu Ruguri.
Aliyasema
hayo Wilayani Tarime mkoani Mara wakati alipokuwa akiendesha harambee ya kuchangia
ujenzi wa ofisi ya jimbo la Mara inayohitaji sh, 2 bilioni ili kukamilika kwa
ujenzi ambapo kwa sasa ipo katika hatua ya orofa ya pili kati ya tano
zinazotakiwa kujengwa.
Katika
harambee hiyo zaidi ya sh, 54 milioni zilitolewa ambapo waumini wa kanisa hilo
viongozi wa siasa toka wilaya mbili za Tarime na Roya walishiriki.
Kiongozi
huyo alisema juhudi za Rais Magufuli kulitoa taifa la Tanzania kutoka katika
mtazamo wa awali wa kiongozi kufumbia macho ufisadi siyo jambo rahisi ambalo
kila mtu atakubaliana nalo hivyo kumwomba asikate tamaa kwa kuwa anamcha Mungu
hakika atafanikiwa, huku akissema kanisa litaendelea kumwombea ili aweze
kufikia malengo yake.
“Ingawa
Musa alikuwa na nia nzuri ya kuwatoa wana wa Israel kutoka utumwani ilifika
wakati baadhi wakamgeukia kumlalamikia kuwa amekuja kuwatesa, vivyo hivyo
kwa Rais namwomba asikate tamaa kwa kuwa kazi anayoifanya ni nzuri na inahitaji
uvumilivu na Mungu atamjalia kuifikisha nchi pale alipotegemea” alisema
Kiongozi huyo.
Awali
akiweka jiwe la msingi katika kanisa la Sabasaba, kiongozi huyo wa kanisa
aliwataka washiriki wa kanisa kuimarisha ujenzi wa nyumba za ibada katika
maeneo yao ili kuifanya sehemu ya kuabudia kuwa bora ambapo Mungu atakaa pamoja
nao.
Aidha
aliwataka hata wale wasiokuwa na uwezo mkubwa kutoa kulingana na uwezo walionao
ili kushiriki mibaraka ya Mungu kwa kuwa Mungu anaona moyo wa anayetoa na sio
wingi wa kile alicho nacho.
Akitoa
shukrani, Mwenyekiti wa jimbo kuu la kaskazini mwa Mwa Tanzania Dkt. Godwin
Lekondayo aliwashuru wananchi waliojitolea kwa kujinyima ili kufaikisha ujenzi
wa ofisi hiyo ambao unahitaji kiasi kikibwa cha fedha na bila kuwa na moyo wa
pekee ujenzi huo hauwezi kukamilika kwa haraka.
Pamoja
na kuendesha harambee hiyo pia viongozi hao walipanda miti ya kumbukumbu katika
kanisa la Sabasaba ambapo pia aliweka jiwe la msingi kwa ujenzi unaoendele,
huku wanawake wa kanisa hilo wakitoa mifuko 10 ya saruji kwa jeshi la polisi
ili iweze kusaidia kukamilisha ujenzi ya ofisi za kituo kikuu cha polisi Tarime
mjini.
|