ZAIDI YA WANACHI 480 KIJIJI CHA MANIRA RORYA WANUFAIKA NA MWANGA WA JUA.
PICHA YA JOHN MASHAKA AMBAYE AMEFADHILI KIJIJI HICHO MSAADA WA MAJI NA MWANGA WA SOLA AKIONESHA SOLA YA MFANO KWA WAANDISHI WA HABRI JANA KIJIJI HAPO. |
RORYA.
Wilayani Rorya mkoani Mara zaidi ya wanachi 480 wa kijiji
cha Manira Kata ya Nyamutinga wamenufaika na Nishati ya Umeme wa jua ambapo
wanachi hao wamesema kuwa suala hilo limeepusha majanga ya kuungua kwa Nyumba
ambayo yaemekuwa yakitokea mara kwa mara kutokana matumizi ya vibatali huku wakivamiwa na wanyama aina ya Fisi na
kusambulia Mifugo nakulazimika kulala
majira ya saa moja ili kujinusuru na fisi hao.
Aidha wanachi hao wamedai kuwa Tangu kuumbwa kwa dunia mpaka
sasa hawajawahi kupata umeme jambo ambalo limekuwa ni changamoto kubwa hivyo
kijiji hicho sasa kinajivunia kupata umeme wa jua huku wakisema kuwa hapo awali
kwa sababu ya giza wamekuwa wakishambuliwa na wanyama aina ya fisi na wakati
mwingine nyumba kuungua kwani nyumba nyingi za vijijini zimejengwa kwa kutumia
nyasi
Issaya Erasto nimmkazi wa kijiji hicho alisema kuwa tangu
kuzaliwa kwake mpka sasa ana umri wa mika 62 hajawahi kuona umeme amekuwa
akitumia vibatali na wakati mwingine kukosa ela ya mafuta na kuamua kuwasha
kuni ili kupata mwanga na kupelekea baadhi ya miji kuungua kwani nyumba nyingi
za vijiji zimejengwa kwa nyasi hivyo ametumia fursa hiyo kumushukuru mfadhili
huyo kwani amewza kuwanusuru wananchi hao.
“Huyu ni kijana wetu tumejinyima kama wanakijiji na kuweza
kumusomesha na kwenda nchi za mbali lakini amekumbuka fadhila na kuweza
kuturudishia kidogo anachopata kwa kushirikiana na marafiki zake wa huku
Marekani Tunashukuru sana sasa watoto wetu watasoma na kufuata nyao zake kwa
sababu kijiji kizima kina mwanga wa kutosha kwani sola hizi hazizimika hata
mvua ikinyesha siku Nne” alisema Issaya.
Kwa upande wake Sofia Mihayo nimmoja wa akina mama alisema
kuwa kijiji kizima wakati mwingine kimekuwa kikikosa mafuta na kuamua kutumia
mishumaa ambayo siyo rafiki kulingana na nyumba zao lakini ujio wa mwanga wa
jua itakuwa chachu ya maendeleo.
Pia wanachi hao walidai kuwa kutokana na giza ambalo
limekuwa likitawala kijijini hapo wanyama aina ya Fisi wamekuwa wakiwashambulia
vikali na kuua wanyama wakiwemo Mbuzi pamoja na kondoo huku watoto wakilazimika
kulala mapema ili wasiweze kushambuliwa na fisi.
Mmoja wa wakazi wa kijijini hapo alidai kuwa baada ya kupata
mwanga wa jua takribani mwezi mmoja watoto wake ambao walikuwa hawajui kusoma
kwa sasa wameanza kujua kusoma hivyo ujio wa mwanga huo katika kijiji hicho ni
neema kubwa.
Hata hivyo mbali na
wanakijiji hao kukumbwa na changamoto ya ukosefu wa umeme maji pia yalikuwa
changamoto kubwa ambapo wakina mama wamekuwa wakitembea zaidi ya kilimeta
ishiri kwenda na kurudi huku wakiamkamajira ya saanane usiku kufuata maji ya
ziwa Victoria ambayo siyo safi na salama
kwa Afya yaho pia kijiji hicho na baadhi ya vijiji Vinne jirani zaidi ya wananchi Elfu Nane
wananufaika mradi wa maji ambao hupo
kijijini hapo chini ya Ufadhili wa John Mashaka Foundation and, American Inginearing Group Limited ambapo katika
kijiji cha manira wameweza kuweka muradi wa maji ambapo muradi huo unahudumia
wanachi wa kijiji hicho pamoja na vijiji Vinne jirani japokuwa wanalipia dumu
la lita 20 shilingi 50 kwa ajili ya matengenezo huku wazee na watu wasiojiweza
wakichota bure bila ya kutozwa chochote.
Miradi hiyo imefadhiliwa na mmoja wa wazawa wa kijiji cha
Manira kata ya Nyamutinga wilayani Rorya Mkoani Mara Bw :John Mashaka kwa kushirikiana na American
Inginearing Group Limited baada ya kuona wananchi wanateseka kwa kukosa huduma
ya maji pamoja na Mwanga huku kila nyumba ikipata mwanga wa jua na zaidi
ya nyumba za nyasi 120 zimenufaika bila kuchangia chochote.
John Mashaka ambaye ni Mfadhili wa miradi hiyo yote alisema
kuwa baada ya kusomeshwa na kuweza kupata kazi Njee ya Nchi aliweza kuamua
kurudi nyumbani na kubaini changamoto zinazokumba kijiji chake na kuamua kuweka
muradi wa maji pamoja na mwanga wa juaili kila mwanachi aweze kunufaika.
“Nilivyokuwa nakuja kijijni kuwapa wanachi wangu Elfu kumi
haisaidii kwa sababu fedha zinaisha na shida zinabaki palepale nikaona nini cha
kuwapa ili kiwanufaishe wote nikaomba marafiki zangu Marekani nakuweza kuniunga
mkono na kufanya hayo muliyoyaona kijijini hapa” alisema Mashaka.
Mashaka aliongeza kuwa muradi huo wa mwanga wa jua umeweza kufikia
kila kaya bila ya kubagua dini wala kabira kwani jamii nzima ilikuwa na hitaji
kubwa la mwanga ili kila family watoto waweze kujsomea na kuweza kufaulu.