Wazazi na walezi wametakiwa kuwa wawazi kwa
mabinti zao waliofikia umri wa kupevuka kwa kuwafundisha mabadiliko ya kimwili
ili waweze kujua jinsi ya kukabiliana na hali hiyo na kujilinda
kutokana na mabadiliko ya mwili badala ya kuwaonea aibu na
kuwaaacha wakiharibikiwa.
Hayo yamebainishwa na mabinti walioshiriki
mkutano wa malezi uliofanyika Manispaa ya Musoma mkoani ukiwa na lengo la
kuwaelimisha akina mama na kuwakumbusha majukumu yao katika familia ili waweza
kuimarisha maadili katika familia zao kwa kuwa wanaukaribu mkubwa na mabinti
tofauti na ilivyo kwa wazazi wa kiume kwa mtoto wa kike.
Miongoni mwa mabinti walioshiriki, Mariam
Jacob alisema wazazi wanaogopa kuwaeleza waziwazi mbinti zao hali halisi ya
mabadiliko ya mwili na mahusiano, hivyo wametakiwa kuwaachia washiriki katika
mikutano kama yeye alivyopata nafasi ili kufundishwa.
“Wazazi wengi wamekuwa wakiwazuia mabinti zao
kushiriki kwenye makongamano ya kujifunza jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya
mwili pindi binti amapobarehe na kuwa chanzo cha wao kuharibikiwa zaidi, hivyo
watoe nafasi yanapokuwepo mikutano kama hii ili washiriki kwani kuna faida
kubwa”.
Na kuongeza “Katika mkutano huu tumegunga
(Vundwa) tumetambua kuwa kuendelea kufanya mambo machafu tunafaninishwa na
inzi, ambaye pia wavulana wanaoturubuni nao wanafananishwa na inzi anayetafuta
chakula mahali popote hivyo tumeelezwa jinsi ya kuepukana nao na madhara
yanayotokea ikiwa tutaingia katika mahusiani na makundi rika” alisema Jacob.
Mtaalamu wa wamasuala ya Mahusiano Elisheba
Mganda alisema vijana wengi walio katika wakati wa kupevuka hasa mabinti,
wanaharibikiwa kwa kukosa ushauri makini na ukaribu wa wazazi au walezi ili
kuweza kuwalekeza nini wapaswa wafanye wakati huo.
Kwa kulitambua hilo idara ya akina mama ya
kanisa la Waadventista wasabato mkoani Mara ikaamua kuitisha mkutano wa
wanawake mkoa mzima hasa wanaosimamia wanawake kupata mafunzo ya jinsi ya
kuwalea familia na watoto wa kike kuepukana na vishawishi vya wanaume.
“Ikiwa binti hatafundishwa haya katika
kipindi hiki cha kupevuka ataingia katika mahusiano kwa muda usiofaa na
kuharibikiwa, wazazi wa kike wana nafasi kubwa ya kuwaambia mabinti kwa uwazi
jinsi ya kuepukana na vishawishi wakati huu wa kupevuka… wakati huu msichana
hupata hamu ya kutamani kukutana na wanaume, maumbo yake huongezeka, huanza
kupendeza na wanaume huanza kumfuatilia, asiposaidiwa hakika huharikiwa na ujue
papai likiiva linahitaji kuliwa” alisema Mtaalamu huyo.
Jumla ya wanawake na mabinti 380 wa mkoa wa
Mara walihudhuria ambapo daktari staafu Hulda Lugoye aliwatahadhalisha
wanaume waliohudhuria kilele cha mkutano huo kuwa wanapaswa kufahamu kuwa
ubongo wa mwanadamu umegawanyika katika makundi matatu ambapo kwa mwanamke
sehemu moja ya katikati (limbic system) ni kubwa kuliko ya mwanaume na ndiyo
maana mwanamke anakuwa na maneno mengi kuliko mwanaume.
“Neo cortex, limb system na brain storm,
zinatofautiana kwa ukubwa ambapo limbic system ya mwanamke ni kubwa kuliko ya
mwanaume na inamfanya mwanamke afanye mambo mengi kwa wakati mmoja kuliko
mwanaume ambaye anafanya kitu kimoja baada ya kingine pasipokuingiliana kwa
hali hiyo sasa mwanamume si mwepesi wa kutoa majibu pale anapoulizwa maswali”
alisema Lugoye.
Na kuongeza “wanawake msiwashutumu wanaume
pale unapouliza kitu anachukuwa muda kukujibu kama unavyotaka wewe ni kutokana
na nafasi ya ubongo inayotoa maamuzi ya kufanya hivyo kufanya kazi kwa umakini
zaidi” alisema daktari huyo.
|