SERENGETI.
TIMU ya Impala ya Serengeti imetwaa ubingwa wa kombe Ruhinda
lililokuwa lililofikia kilele chake juzi jumapili kwa kuitandika Kibeyo FC
kukubali kichapo cha 1-0 kwenye fainali za kombe hilo zilizofanyika katika
uwanja wa shule ya Msingi Matere mjini hapa.
Ligi hiyo iliyoanza june 6 ilifikia kilele chake juni 12
ikishirikisha timu sita ambazo ni Kibeyo, impala, Imara, Itununu, Wasanii na
Park land.
Bao pekee la ubingwa la Impala FC lilifungwa na Tito James
katika dakika ya 2 ya kipindi cha kwanza na kuwafanya Kibeyo FC kupoteza
mwelekeo wa mchezo huo baada ya kuwahiwi na wapinzani wao.
Kocha wa Kibeyo FC Pius Kikondo ameiambia CLEO NEWS kuwa
kufungwa katika dakika ya pili kuliwafanya wachezaji wake kuchanganyikiwa
na kushindwa kumudu mchezo huo ambapo walilazimika kuzuia ili wasiongezewe bao
la pili jambo ambalo walifanikiwa huku wakishindwa kusawazisha.
“Makosa yalifanyika mapema tu tulipoanza mchezo na wapinzani
wetu wakatumia mwanya huo kutufunga kutokana na wachezaji wangu wengi kuwa
wageni wa soka hawajawahi kushiriki katika ligi kubwa ya timu sita kama
hii,hata hivyo mchezo ndivyo ulivyo na matokeo yake ndivyo yalivyo usiposhinda
unashindwa wewe” alisema Kikondo.
Kwa upande wake kocha wa Impala FC ya Matare, Lucas Pius
alisema ushindi wao ulitokana na kuiandaa timu yake mapema baada ya kukabidhiwa
kama kocha mwaka jana mwezi wa nane na kusema lengo lake ni kuiweka
katika kiwango kizuri cha kuipandisha kutoka daraja la nne hadi daraja la tatu
ngazi ya mkoa.
“Mazingira na uhaba wa vifaa ni moja ya changamoto
zinazifanya timu nyingi kutofanya vizuri katika michuano mbalimbali, kuendesha
timu kunahitaji pesa lakini nashukuru Impala FC kwa kuonyesha moyo wa kujituma
hadi kufikia kuwa mabingwa wa kombe la Ruhinda na niwaahidi mashabiki wangu
kuwa bado yapo mengi ya kuwafurahisha niliyowaandalia” alisema Pius.
Mratibu wa michuano hiyo, Daniel Solomon alisema kuwa
mshindi wa kwanza alijinyakulia ngao, pesa taslimu sh, 50,000 na mbuzi beberu,
huku mshindi wa pili akijitwalia cheti cha ushiriki na sh, 30,000 na mshindi wa
tatu ambaye ni Itununu alipata sh, 20,000 na cheti.
“Kila timu iliyoshiriki imepata cheti, huku zawadi zingine
zikiwa ni kwa mfungaji bora Emmanuel Amos amepata cheti, timu yenye nidhamu
iliyoenda kwa timu ya Wasanii na golikipa bora Marwa Amos wa Impala
FC amepata Cheti” alisema Solomon.
|