Walimu wa mpira watakiwa kuwa wabunifu.
Walimu wa mpira nchini wametakiwa kuwa wabunifu katika mbinu za ufundishaji ili kuwafanya wachezaji kuwa na uelewa mkubwa wa mchezo huo huku wakiwapa nafasi ya kushiriki kutoa mawazo ya ya jinsi ya kuboresha mchezo huo kuliko wao (makocha) kuwa na maamuzi ya jumla ya nini kifanyike.
Hayo yalibainishwa juzi hivi karibuni na Graham Robinson kocha wa klabu ya
Sunderland (AFC) ya uingereza wakati wa kozi ya siku tano ya makocha kiwango cha
CAF iliyoandaliwa na mgodi wa Acacia north Mara na kufanyikia katika shule ya
sekondari Ingwe iliyoko Nyamongo Tarime mkoani Mara.
Jumla ya makocha 22 kutoka shule za msingi, sekondari,
vijiji vinavyouzunguka mgodi huo walishiriki kozi hiyo kwa siku tano, kwa njia
ya vitendo na nadharia ambapo jumla ya vijana 200 walijitokeza kuwa sehemu ya
kujifunza mbinu mbalimbali za kupokea, kugawa pasi mpira na jinsi ya kumchenga
adui.
Robinson alisema kuna makocha wengi wenye uwezo wa
kufundisha timu za kimataifa lakini hawajapata mafunzo yanayoweza kuwaweka
katika kiwango kizuri na kuahidi kushirikiana na kampuni ya Acacia Tanzania ili
kutumia muda wake kuhakikisha wanapatikana makocha wenye uwezo watakao weza
kufundisha ngazi ya kimataifa.
“Natamani nami kuwa sehemu ya waafrika mna uwezo mkubwa wa
kuelewa haraka na kufanya kwa vitendo, nishukuru mgodi wa acacia kwa kuona
umhimu wa kuandaa kozi hii kwa kukishirisha klabu ya Sunderland kuyatoa, nasi
kama Sunderland tunaahidi kuwa tutahakikisha wanapatikana makocha wenye kiwango
kizuri na kusimamia pia kupata vyeti kupitia TFF” alisema Robinson.
Kwa niaba ya mkuu wa mgodi huo, Afisa mahusiano wa mgodi huo
Fatuma Msumi alisema lengo la mgodi huo kuandaa kozi hiyo ni kutaka kuinua
viwango vya ukocha katika wilaya ya Tarime hasa karibu na migodi ili iweze
kutoa timu imara.
“Tunahitaji kupata timu imara na yenye uwezo mzuri wa soka
katika maeneo yetu ya wilaya ya Tarime itakayoleta sifa, mwanzoni tulikuwa na
timu ya Nyamongo FC iliyofikia ngazi ya ligi daraja la tatu mkoa lakini badaye
ikaanza kusuasua kutokana na kutokuwa na makocha wenye uwezo na ndio maana
tukaona tushirikiane na klabu ya Sunderland kutoa mafunzo hayo na
tuwashirikishe watu wa kada mbalimbali pia” alisema Msumi.
Washiriki wa kozi hiyo walisema wamejifunza vitu
ambavyo walikuwa hawa vifahamu na kutokana na hali hiyo wataboresha ufundishaji
wao katika maeneo husika ili kuibua vipaji kwa vijana wadogo na timu kubwa kwa
ajili ya michezo mbalimbali ya Wilaya, mkoa na kitaifa pia.
“Sikufahamu kuwa kocha anatakiwa kuwauliza wachezaji ni nini
wannapenda wafanye, nilikuwa nikiamua nini wafanye badala ya kuwapa nafasi ya
kutoa mawazo yao jambo ambalo hapa nimeliona ni zuri ili kuwashirikisha
wachezaji na kuongeza ufanisi wa kikosi kiwapo uwanjani, maana wachezaji nao
wanauwezo mzuri wa kushauri na kufanikisha mchezo uwanjani” alisema Emmanuel
Nyanyembe kocha wa ABG FC.