WAWILI WAFA KWA AJALI YA GARI NA MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA MAWE.


Watu wawili  wamefariki dunia wanne wajeruhiwa kutokana na ajali baada ya gari walilokuwa wamepanda kuacha njia na kupinduka  huku mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la  George Athuman Mwita 27  mkazi wa kijiji cha kerende wilayani Tarime aliuawa kwa kupigwa na Mawe na wanachi wenye kujichukulia sheria mkononi baada ya marehemu kumjeruhi  mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la  Marengo Mwita 32 mkazi wa kijiji cha kewanja kwa kumkata na panga mkono wa kulia kwa sababy ambazo hazijajulikana.

Kamanda wa polisi Mkoa wa kipolisi  Tarime Rorya Andrew Satta amedhibitisha kutokea kwa matukio hayo huku akisema kuwa tukio la kwanza  la gari  aina ya Misitubishi Canter yenye namba za usajiri T 937DFG mali ya Edward John  mnamo tarehe 6 06 2016  katika barabara itokayo shirati –Tarime kitongoji cha Nyawita  kijiji cha Lolwe Kata ya Kinyenche Tarafa ya Nyancha Wilayani Rorya mkoani Mara gari hili likiwa limebeba  abiria sita  likitokea shambani kubeba mazao lili acha njia na kupinduka na kusababisha vifo vya wati wawili papo kwa papo na watu wanne kujeruhiwa.

Kamanda amewataja walikufa kuwa ni Godfrey Sila mjaluo 30 mkazi wa nyamisambala, Ponsian Vitus 40 muha  mfanya bihasara na mkzi wa Tarime na Majeruhi ni Esther Julius  27 mkurya na mfanya bihashara mkazi wa  Tarime Marwa Makuli mkurya35, Shimo Lameck 25 na Giribe John Mfanyabihashara wote ni wakazi wa Tarime Mkoani Mara.
Majeruhi hao wamelazwa katika Hospitali ya KMT Shirati kwa  matibabu na miili ya marehemu imeifadhiwa hospitalini hapo Dereva ametoroka baada ya ajali hiyo na juhudi za kumutafuta zinzendelea na chanzo cha ajali ni mwendo kasi.

Tukio linguine kamanda amesema kuwa  mnamo tarehe 06 06 2016  katika kitongoji cha nyamikoma kata ya Matongo Tarafa ya Ingwe Wilayani Tarime Mkoani Mara  Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la George Athuman 27 mkurya na mkulima mkazi wa kijiji cha Kerende aliuawa kwa kupigwa mawe sehemu mbalimbali za mwili wake na kumusababishia kifo na wanachi wenye kujichukulia sheria mkononi.

Chanzo cha tukio hilo ni  Marehe baada ya kumjeruhi mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la  Marengo  mwita 32  mkurya mkulima na mkazi wa kijiji cha  Kewanja Wilayani Tarime Mkoani Mara kwa kumkata na panga mkono wa kulia  kwa sababu ambazo hazikujulikana.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya Andrew Satta  ametoa wito kwa wanachi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake wafikishe mtuhumiwa katika vyombo vya  sheria huku akiwataka madereva wa vyombo vya moto kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka vifo vya mara kwa mara na baadhi yao kubakia vilema wa kudumu.




Powered by Blogger.