WATU wanne wilayani
Tarime mkoani Mara wamefariki dunia kwa
matukio tofauti likiwamo la watatu kufa kwa kuchomwa kisu tumboni na shingoni huku
mwingine akilazwa hospitali ya
wilaya na mtu mwingine amekufa kwa
kunyongwa ambapo chanzo cha matukio hayo ni wivu wa kimapenzi,Ugomvi ambapo marehemu wengine chanzo cha vifo vyao havijafahamika ,matukio
yote hayo yametokea ndani ya siku mbili huku mwanafunzi wa shule ya Msingi wa
miaka 14 akibakwa na kusababishiwa
maumivu makali.
Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya ACP. Andrew Satta alithibitisha kutokea kwa
matukio hayo ,alisema kuwa mnamo Juni
5,2016 majira ya saa 2 usiku barabara ya Mogabiri Kata ya Kenyamanyori Wilayani Tarime ,Daniel
Masubo (20) mkazi wa Mogabiri
alijeruhiwa kwa kuchomwa kisu shingoni karibu na koromeo na Steven Mniko
(30) mkazi wa kijiji hicho ambaye nayeye alijeruhiwa kwa kisu shingoni.
Kamanda Satta alisema kuwa Majeruhi wote walifikishwa
hospitali ya wilaya ya Tarime kwa matibabu na ilipofika majira ya saa 4 usiku
Daniel Masubo alifariki dunia akiwa anaendelea na matibabu na chanzo cha tukuo ni
baada ya marehemu kumaliza shughuli zake Mogabiri senta wakati akienda nyumbani
kwake akiwa anaendesha pikipiki yake kwa bahati mbaya alimgusa mtuhumiwa.
Satta aliongeza kuwa
baada ya mtuhumiwa kuguswa ndipo ugomvi ulipoanza na kuanza kushambuliana kwa
visu nakwamba mtuhumiwa amelazwa katika hospital ya Wilaya Tarime kwa matibabu
chini ya ulinzi wa polisi na atafikishwa mahakamani mara atakapopata nafuu.
Kamanda Satta anaeleza tukio lingine Juni 3,2016 katika
kitongoji cha Kitare kijiji cha Kimusi
kata ya Nyamwaga wilayani hapa Gikaro
Magaigwa (32) mkazi wa kijiji cha kimusi aliuwawa kwa kwa kuchomwa kisu tumboni
upande wa kulia na kiganja cha mkono wa kushoto na Babere Mniko na chanzo cha tukio hilo hakijajulikana na
mtuhumiwa alikimbia na anatafutwa na Polisi.
Satta alisema tukio lingine limetokea Juni 3,2016 katika kitongoji cha
Bubiritocho kijiji cha Borega “B” Kata ya Mbogi Gimonge Chacha (20) mkazi wa
kijiji hicho alijeruhiwa kwa kuchomwa kisu tumboni na Mwita Taisamu, majeruhi
alilazwa hospitali ya mkoa wa Mara na hali yake ni mbaya na mtuhumiwa alitoroka
kabla hajakamatwa na chanzo cha tukio hakijafahamika.
Hata hivyo mwenyekiti wa kijiji cha Borega B. Omari Juma
alisema kuwa “ Marehemu alichomwa kisu wakiwa arusini na alifariki akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Musoma na chanzo cha kifo ni baada ya marehemu
kumtania mtuhumiwa kuwa bibi arusi alikuwa ni Demu wake na amekula pesa yake sh.5,000 na atammisi
sana kwakuwa kaolewa na walizidi
kutaniana mwishowe kukazuka ugomvi na
kumchoma kisu marehemu”alisema Mwenyekiti wa kijiji.
Sata alisema tukio
lingine Mkazi wa kitongoji cha Matoke
kijiji cha Mangucha kata yaNyanungu wilayani hapa Lameck Makanga(45) aliuwawa
kwa kunyongwa na kamba shingoni na mtu/watu wasiofahamika saa tisa jioni na kwamba Jeshi la Polisi
linamshikiria Rhob Makanga,(30) kwa
mahojiano zaidi kwakuwa taarifa za awali zinaonyesha kuwa kulikuwa na ugomvi
kati ya marehemu na mke wake hiyo.
Satta alisema kuwa marehemu alikuwa anamtuhumu mke wake huyo
mdogo kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine na hivyo kupanga
njama na watu wasiojulikana na kumyonga.
Wakati huohuo, Mwanafunzi
wa darasa la sita wa miaka (14) katika shule ya msingi Bag iliyopo Nchini Kenya
ambaye ni mkazi wa Buriba kata ya Sirari wilayani hapa amebakwa na Kelvin
Nyambuga(22) ambaye ni fundi ujenzi na mkazi wa kijiji hicho cha Sirari na
kumsababishia maumivu makali.
Satta alisema kuwa tukio hilo lilitokea juni 5,2016 majira
ya saa 11 jioni huko kitongoji cha Nyasoko kata ya Sirari nakwamba myuhumiwa
amekamatwa na mara baada ya mahojiano atafikishwa mahakamani.
|