Wafanyabishara
wa mbogamboga, na viazi vitabu katika soko la Sirari wilayani Tarime mkaoni
Mara, wameitaka serikali kuwaondolea ushuru wanaotozwa njiani sokoni wakati
wanatoka kuchukua bidhaa ili kuwapunguzia mzigo na hasara inayopatikana kwa
kukosa wateja wa bidhaa zao.
Waliseama
kuwa tozo hizo za njiani na sokoni hutozwa wakati wakitoka kuchukua mzigo
na wanapofika sokoni pia hutakiwa kulipia ushuru wa soko hivyo kuwafanya
wasipate faida kutokana na kukosa wateja na viazi na mboga kuchukuwa muda mrefu
kununuliwa na kupoteza mvuto kwa wateja wao.
Wakizungumza
sokoni hapo na Cleo news hili akina
mama hao walisema kuwa gunia moja la viazi vitamu lenye uzito wa kilogram 90
wanalinunua kwa sh, 20,000 na kulisafirishia kwa nauli y ash, 1,500 huku
wakitozwa sh, 500-1000 wakiwa njiani na wanapolifikisha sokoni hutozwa sh, 500
kila jumamosi ambayo ni siku ya soko, hivyo hawapati faida.
“Gunia
hilo unaliuza wiki nzima, viazi vikinyauka tunapata hasara na ndiyo
tunayoitegemea kutunzia familia watoto kuvaa na kula na wengine kulipiwa shule
maana sisi hapa tuko mpakani watoto wanasoma hapo Kenya, tunaomba ushuru
upunguzwe ili tupate unafuu” alisema Esther Sililo.
Muuzaji
wa viazi sokoni hapo, Marselina Wambura alisema wanapata shida ya kuungua na
jua hivyo kuitaka serkali kujenga vibanda kwa ajili ya kuwasaidia kujikinga na
jua, mvua na upepo pale wanapokuwa sokoni kwa kuwa wanalipa ushuru.
“Tunaungua
jua sana kutokana na kuwa hakuna vivuli vya kutukingia jua, tukipata vichanja
biashara yetu itaenda vizuri… tukiwa na sehemu moja wote tunaouza biashara hizi
tutapata faida kubwa huku waturuhusu tuvushe kwenda kenya maana kuna soko zuri”
alisema Wambura muuzaji wa viazi.
Walisema
kuwa wakiboreshewa mazingira kwa kupangwa katika maeneo maalumu kutawafanya
wateja wao kupata huduma katika sehemu husika.
“Tunaomba
maeneo yatengwe kufuatana na aina ya biashara tunayofanya yataturahisishia kazi
yetu na kutunza maeneo kuwa safi, kama ni viazi tuwe na eneo letu, kuku, mkaa
na matunda kuliko ilivyo sasa tumechanganyikana pamoja na wauza kuku mkaa vitu
vingine” anashauri Silvia Bajunana
Ili
kuboresha mazingira ya soko hilo la mji mdogo wa Sirari, halmsahauri ya Wilaya
Tarime kupitia mfuko wa jimbo imetenga zaidi y ash, 9. Milini kujenga vichanja
vitakavyotumiwa na wafanyabiashara katika soko hilo na kuondokana na kuweka
bidhaa zao chini.
Katibu
wa mbunge wa jimbo hilo Mrimi Zabron alisema tayari pesa hiyo imetengwa na
utekelzaji wa ujenzi wake unatarajiwa kuanza mara moja baada ya kukamilisha
masuala machache yaliyobaki kukamilishwa.
Katika
kata ya Sirari imetengewa sh, 9 milion kwa ajili ya utengenezaji wa
vichanja vya kisasa kwa ajili ya kinamama wajasiriamali zitakazowasaidia kuuzia
mboga na samaki na mazao mengine ya bishara katika soko la Sirari ambapo jumla
ya sh, 40,295,000 milioni zinatekeleza miradi ya ukarabati ya shule za
msingi wilayani Tarime” alisema Zabron.
|