WAISLAMU WATAKIWA KUSAIDIA JAMII.
Hayo yamebainishwa na Sheikh wa kata ya Tarime Mjini Tawfiq
Khamis Hussein baada ya kutembelea Gereza la wafungwa Wilayani Tarime mkoani
mara na kutoa msaada wa chakula, ikiwemo Sukari Mafuta ya kula, na Mchele ili
waumini wa kiislamu ambao wako ndani ya gereza waweze kushiriki vyema mwezi
mutukufu wa ramadhani.
Aidha Sheikh Huyo alisema kuwa waumini wa kiislamu wana haja
kubwa kuendelea kusaidia waumini wenzake pamoja na watu wasikuwa waumini ikiwa
ni pamoja na jamii nzima kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsi pamoja na
udhalilishaji kwani maandiko matakatifu yanakataza matendo hayo.
“Wilaya ya Tarime na Nchi kwa ujumla kumekuwepo na vitendo
vya kinyama pamoja na udhalilishaji hivyo jamii haina budi kumwogopa mwenyezi
mungu” alisema Sheikh.
WATA) Ramadhan Katura alisema kuwa
lengo la kuwatembelea wafungwa hao ni jukumu lao kulingana na maandiko yanavyosema
na kudai kuwa siyo mwisho bali wataendelea kuwatembelea na kutoa kidogo
wanachopata kutoka kwa mwenyezi Mungu.
Hata hivyo Katibu Huyo alisema kuwa katika kumaliza mwezi
mutukufu wa ramadhani wanaona jinsi gani wafungwa hao wataweza kushiriki na
waumini wenzao ambao wako uraiani ili kuwa na furaha na kuonesha kuwa mwenyezi
mungu yuko nao.
Kwa upande wake kaimu mkuu wa Gereza la wilaya ya Tarime Kilulu Lucas
alisema kuwa suala hilo la waumini wa kiislamu kutembelea gereza hilo
linazidi kuwatia moyo wafungwa hao na mahabusu kuwa kuwa magereza siyo kwamba wametengwa na mwenyezi Mungu huku akitoa wito kwa waislamu hao kuendelea kuutumia vyema
mwezi mutukufu wa ramadhani kama kusudi lao.
Bashir Abdalah ni mmoja kati ya waumini wa kiislamu amesema
kuwa katika mwezi mutukufu wa ramadhani
wameupokea vyema huku wakiomba wafanya bihashara Wilayani Tarime mkoani mara
kutopandisha bei za vyakula waumini wa kiislamu kuendelea kuvaa mavazi ya
heshima yanayompendeza mwenyezi mungu.
“Kwa kuwa ni mwezi mutukufu wa ramadhani sasa tunaomba
wafanyabiashara wasitumie mwanya huu kupandisha bei baadhi ya viyu ikiwemo
chakula Sulari na vitu vingine” alisema Bashir.