WAJASILIAMALI WATAKIWA KUPEWA KIPAUMBELE.
Akina mama wajasiliamali nchini wametakiwa kupewa
kipaumbele kwa lengo la kulikomboa Taifa kiuchumi ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha wanakabiliana na changamoto zinazo wakabili ikiwemo ukosefu wa mitaji
hali inayowafanya akina mama wengi kushindwa kujikimu na kuanzisha miradi
mbalimbali ya ujasilia mali kutokana na hali duni inayozikumba familiya nyingi
nchini .
Wakizungumza changamoto zinazowakabili na kutoa akina mama wajasiliamali mkoani mara katika warsha ya kufunga mafunzo ya siku mbili
ya urasimishaji wa biashara ya vyanzo vya fedha kwa wanawake wajasiliamali
yakiwemo majukwaa ya wanawake ya ujasiliamali
iliyofanyaka wilayani Tarime mkoani mara walisema kuwa serikali haina
budi kutambua uwepo wake na kuwawezesha mikopo kwa lengo la kuedeleza miradi
yao.
Aidha akina wajasiliamali hao walidai kuwa wamekuwa
wakijishughulisha kwa lengo la kujikwamua lakini bado wanakumbwa na changamoto
ya ukosefu wa mitaji huku wakiomba mabanki kutoa mkopo yenye riba nafuu ili
kila mtu aweze kufanya biashara.
“Tunataka kufanya biashara kupitia vikundi kwa
sababu akina mama wengi familia zinatutegemea lakini bado tunakumbwa na changamoto
ya ukosefu wa mitaji bado banki zinatoa mikopo kwa riba kubwa jambo ambalo
linawashinda akina mama wengi kuchukua mikopo” walisem akina mama hao.
Akisoma risala mbele ya mkuu wa wilaya ya Tarime
Glorious Luoga mwenyekiti wa jukwaa la wanawake la kiuchumi,TANZANIA WOMAN
CHAMBER OF COMMERCE (TWCC) mkoa wa mara Safia
Chacha amezitaja changamoto zinazo wakabili ikiwemo ukosefu wa mitaji ,
mazingira yasiyorafiki kwa biashara na huku akizitaja changamoto zingine
zinazochangia wao kutopiga hatua .
Akieleza lengo na fursa za majukwaa ya wanawake ya
kiuchumi nchini Tanzania mkurugenzi mtendaji wa TWCC Flora Rimoy alisema kuwa
kupitia jukwaa la kina mama hilo kwa kiasi furani linazidi kuwakwamua wanawake
wengi Tanzania ambapo amesema kuwa wana mikakati ya lkufungua majukwaa mengi
kila mikoa ili kuwasaidia akina mama hao wajasiliamali.
Naye katibu wa TWCC Mkoa wa Mara Noela Gachuma alongeza kuwa kuwepo kwa jukwaa hilo ni kuweka sauti ya
pamoja na kushirikiana na kupeana mawazo kwa lengo la kumkomboa mwanamke wa
Tanzania .
Akifunga mafunzo ya semina hiyo kwa akinamama
wajasiliamali mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Luoga amekiri kupokea
changamoto hizo na kuanza kuzifanyia kazi huku akitoa kalipio kali kwa wale
wanaowanyonya na kuwakandamiza wajasilamali hao huku akigusia taasisi za kifeza
zinazowanyonya wajasilamali kwa riba kubwa
.
Hata hivyo mkuu wa wilaya huyo aliwataka
wajasiliamali hao kujikita katika suala zima la kufuga kuku wa kisasa ili kuwa
na miradi ya kuuza mayai na kudaia kuwa endapo wajasiliamali hao wataanzisha
muradi atakuwa wa kwanza kuwatafutia soko la kudumu.
“Kwanza wafanyabiasara akina mama wa Tarime mna
bahati nzuri kuna mgodi wa ACACIA pamoja na Mbuga za Wanyama kupitia wawekezaji
hawa hata mukiwa na mayai maelefu yataisha na kuitajika mengine hivyo ni jukumu
lenu kujipanga sasa ili kumaliza umaskini nyie ndo mmekumbatia umaskini fursa
ni nyingi pia mpaka hupo lakini hamujabuni miradi ili kunufaika”alisema Mkuu wa
Wilaya .
Kauli mbiu na dira ya mafunzo hayo ikiwa ni “kua
kitovu na kichocheo katika kumkomboa
mwanamke mfanyabiashara wa kitanzania kiuchumi ”.