DC RORYA MADIWANI ENDELEA KUSISITIZA KILIMO CHA MIHOGO NA UFUTA.
Rorya
Mkuu wa
wilaya ya Rorya Felix Lyaniva amewataka madiwani kuasa wanachi kuendelea kulima kilimo cha
Mihogo pamoja na ufuta kwa ajili ya zao la biashara huku madiwani hao wakiwa na
mashamba Darasa kwa lengo la kukabiliana na njaa ambayo imekuwa ikikumba wilaya
ya Rorya Mkoani Mara huku Mkuu wa wilaya huyo akiwataka watendaji kuweka
utaratibu ili wanachi wasiuze vyakula na pale watakapovuna waweze kutunza
chakula hicho kwa lengo la kukwepa njaa.
Aidha mkuu
wa wilaya uyo amesema kuwa wakulima
wilayani Rorya hawana budi kuendelea na zao la mihogo kulingana na agizo
alilotoa mkuu wa Mkoa kuwa kila Mwanachi apande zao hilo ili kukabiliana na
njaa ambao mara nyingi imekuwa ikikumba wilaya ya Rorya huku akiwataka wanachi
wasiuze chakula na kumaliza majumbani.
Hata hivyo
mkuu wa wilaya huyo amewataka Wenyeviti pamoja na watendaji wa vijiji na kata kwa kusirikiana na madiwani kuweka mikakati na
utaratibu wa uhuzaji wa chakula kwa
wanchi kwani kuna baadhi ya wanachi wanauza chakula mpaka familia inaishiwa na
badae wanakumbwa na njaa hili suala sitakubaliana nalo.
Hata hivyo
mkuu wa wilaya huyo amewataka madiwani hao kuwa na mashamba darasa kwa ajili ya
mifano mi. na kuendelea kuhamasisha wananchi hao kuendeleza kilimo hicho
kikiwemo kilimo cha Ufuta kwa ajili ya biashara ili kujikwamua kiuchu.
Wakiuliza
maswali ya papo kwa papo madiwani hao katika balaza la kawaida lilofanyika
wilayani Rorya Mkoani Mara Lazaro
kitori ni diwani wa kata ya mukoma Wilayani
rorya kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA amesema kuwa
Halmashauri ya wilaya ya Rorya kutokana na kuchelewesha uchaguzi wa mamlaka ya
mji mdogo wa shurati unazidi kupelekea baadhi ya mambo kukwama na kuwamisha
maendeleo ya wanachi pamoja na ukuaji wa mji huo huku akiomba Halmashauri hiyo
kurejesha vijiji vilivyokuwepo hawali ili vikao viendelee kwa ajili ya
maendeleo.
Akijibu
Swali hilo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya Charles Chacha amesema kuwa
wanaendelea na utaratibu mpka sasa zimebaki hatua Nne huku akisema kuwa jambo
linalowasumbua ni vyanzo vya mapato watakapoanzisha mamlaka ya mji mdogo huo.
Kwa upande wake Katibu Tawala Wa Halmashauri
ya wilaya ya Rorya Daud Mulumbe amewataka madiwani hao kuaminiana na kushauri
wanachi kubadili fikra pamoja na mitazamo huku madiwani hao wakiondokana na
kukuza mabo ambayo yanaweza kuhatarisha maisha ya Wanachi.