JAMII YALAANI KITENDO CHA MWANAMME KUMKATA MKEWE KWA PANGA SHINGO.
JAMII YALAANI KITENDO CHA MWANAMME KUMKATA MKEWE KWA PANGA
SHINGO.
Kulingana
na vitendo vya ukatili ambavyo vinaendelea kushamili hapa Nchini kwnye maeneo mbalimbali, Katika hali isiyo ya kawaida
Wilayani Tarime mkoani Mara Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Wambura
Maningo Mrimi 50 mkazi wa kitongoji cha Nyabirama kijiji Matongo wilayani hapa amemua mkewe aitwaye Maria Wambura Maningo 38
kwa kumkata kichwa kwa panga moja kutoka kichogoni hadi shingoni na kufariki
papo hapo.
Tukio
hilo lilitkea manamo Juni 08 Mwaka huu majira ya saa Tisa Mchana ambapo kipindi
mwanamke huyo anaandaa chakula cha machana ndipo mmewe alimtokea kwa nyuma
akiwa na panga mkononi na kumkata Kwenye Kichogo na kumusababishia kifo papo
hapo.
Aidha
bada ya kutenda tukio hilo la Kinyama mtuhum,iwa huyo alichoma nyumba zake
mbili za nyasi kwa moto na mali zote ambazo hazikufaamika thamani yake na
kuteketea.
Ni
vilio simanzi taharuki katika mji mdogo wa Nyamongo kwa tukio ambalo limeacha wakazi
wa nyamongo na vitongoji vyake mdomo wazi wasijue la kusema na kufanya baada ya
kutokea mauaji ya kinyama kwa mume kumuua mkewe kwa kumkata kwa panga moja tu
kutokea kichogoni na kukatika shingo bila habari wakati akiandaa chakula cha
mchana huku wanachi hao wakitaka kumuua kama alivyofanyakitendo hicho cha
kinyama lakini jeshi la polisi lilweza kuingilia kati na kuokoa maisha ya huyo
mtuhumiwa.
“Nasisi
ni haki yetu kumaliza maisha ya huyu baba sasa familia amehiacha na nani na
serikali inamuchukua bora sasa ikamuhukumu kufungwa maisha au kunyongwa” hayo
yalikuwa na maneno ya wanachi baada ya tukio hilo la kinyama.
Kamanda
wa mkoa wa kipolisi Tarime Rorya Andrew Satta amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari mtuhumiwa
alikamatwa siku hiyo hiyo huku na mtuhumiwa huyo amelazwa akiwa katika ulinzi
mkali wa jeshi la polisi katika
hospitali ya mji wa Tarime kwa matibabu kwani wanachi hao walimushambulia na
kumjeruhi na kitu chenye Ncha kali shingoni baada ya unyama huo na baada ya
kupata nafuu atafikishwa mara moja mahakamani.
Chanzo cha tukio hilo ni imani za kishirikina kuwa mke wake ambaye sasa ni marehemu alikuwa
akimuloga mtuhumiwa huyo.
Kaijage
kagumilwa ni mganga mkuu mfawidhi wa kituo cha afya Nyangoto ambapo mwili wa
marehemu uliifadhiwa baada ya kufanyiwa kitendo cha unya na kusema kuwa kwanini
jamii imekuwa ikiendelea kutenda unyama huu sualaambalo limewashangaza kutokana
na tukio hilo la kinyama.
“Matukio
ni mengi tunayopokea hapa lakini mengine hata hayalipotiwi sas tunakoelekea ni
wapi” alisema Kagumilwa.
Hivyo
kutokana na matukio hayo ya kinyama kushamili kuna haja kubwa ya serikali
kuliona hilo na kutunga sheria kali dhidi ya watu ambao wamekuwa wakifanya
vitedo vya ukatili na kuendelea kuchafua Taifa la Tanzania.