CORD yatangaza majina ya watano watakaotumika kujadili swala la IEBC

Muungano wa CORD umetanagza kundi la watu 5 ambao watatumika kwenye mdahalo kuhusu swala tata la kuwepo afisini makamishna wa IEBC. Katika taarifa kwa vyombo vya habari watau nao ni Seneta wa Siaya James Orengo, Seneta wa Machakos Johnstone Muthama, mbunge wa Tongaren Dkt Eseli Simiyu. Mwakilishi kinamama kaunti ya Momabsa Mishi Mboko na mbunge wa Balambala Abdikadir Aden. Watano hao watafanya kazi kwa ushurikiana na makatibu Paul Mwangi na Grace Katasi. Kundi hilo limetangazwa siku moja baada ya CORD kuahidi kufanya hivyo wakati wa mkutano wao ulioandaliwa jana bustani ya Uhuru.

Powered by Blogger.