KUANZA kwa Chuo Kikuu cha Kilimo na Sayansi cha Mwalimu Julius
K.Nyerere,kilichopo wilayani Butiama mkoa wa Mara kitaupandisha na kuuinua mkoa
katika masuala mbalimbali pamoja na kuwasaidia wakulima katika kuinua kilimo.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Mara,Magesa Mulongo,alipotembelea
sehemu ya majengo ya iliyokuwa shule ya Osward Mang'ombe High School ambayo
yatatumika kama "campas"ya chuo hicho kinachotarajiwa kuanza kupokea
wanafunzi oktoba mwaka.
Amesema chuo hicho ambacho kitatoa shahada na stashahada za fani mbalimbali
licha ya masuala ya kilimo itakuwa chachu kubwa ya maendeleo ya mkoa wa Mara na
wananchi watakaokuwa wanazunguka mazingira ya chuo na kuwataka wananchi
kujiandaa kukipokea.
Mulongo ambaye alikuwa ameongozana na viongozi wa ngazi ya wilaya,alisema
cha kwanza ambacho kinapaswa kuangaliwa ni kuhakikisha migogoro ya aina yoyote
baina ya chuo na wananchi haipatikani yakiwemo masuala ya ardhi ili
uongozi wa chuo ufanye shughuli zake bila kubugudhiwa.
"Kwanza ni heshima kubwa kuwepo na kuletwa kwa chuo hiki mkoa wa Mara
na hususani kwenye wilaya ya Butiama katika kumuenzi mzee wetu Mwalimu Julius
Nyerere na ni muhimu kinapokwenda kuanza kusiwepo na vikwazo vya aina yoyote.
"Lakini chuo hiki kitaupandisha na kuuinua mkoa wa Mara maana mahala
popote palipo na vyuo au chuo kikuu licha ya mkoa kunufika lakini pia wananchi
wananufaika kutokana na fursa mbalimbali ambazo watazipata kutoka kwa
wanachuo,"amesema Mulongo.
Amesema kutokana na taarifa ambazo amepewa na uongozi wa chuo
hicho,wananchi wakulima wa kawaida pia watapata fursa ya kupata kozi fupi
ambazo zitawasaidia kuboresha shughuli zao za kilimo na kuwaomba wananchi
kujiandaa na hilo.
Akitoa taarifa ya chuo hicho baada ya kuteuliwa na Rais wa awamu ya
nne,Jakaya Mrisho Kikwete,kuanza mchakatato wa chuo hicho,Naibu Makamu Mkuu wa
Chuo Taaruma,profesa Lesakit Mellau,amesema wameshafikia hatua kubwa ya kuanza
kwa chuo hicho ikiwemo kuanza kuajili wahadhiri.
Amesema bado kuna masuala ya fedha kutoka serikalini yasubiliwa kutokananza
kupokea na bajeti na mambo yakienda vizuri kufikia oktoba wataanza kupokea
wanafunzi.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Butiama waliozungumza na CLEONEWS
kuhusiana na chuo hicho walisema wapo tayari kutoa ushirikiano kutokana na
manufaa ambayo watayapata kutokana na kuwepo kwa chuo hicho katika maeneo yao.
|