MAMBA, FISI TISHIO KWA WANACHI MURITO.
MAMBA, FISI TISHIO KWA WANACHI MURITO.
Wananchi wanaoishi kijiji cha Murito Wilayani Tarime wanakabiliwa na tishio la mamba na fisi wanaowashambulia na mifugo nyumbani na wawapo mtoni wakiwajeruhi na kuwaua.
Mtu mmoja ameuwa na wengine sita wakijeruhiwa na mamba na kuachwa na vilema vya maisha huku mifugo zaidi ya 50 ikiuawa kwa kipindi cha mwaka jana unaoishia mwezi mei mwaka huu 2016.
Hata hivyo mkurugenzi wa halmashauri ya Tarime athuman Akalama amesema hana taarifa zozote kuhusu madai ya wananchi na viongozi wa kijiji cha Murrito lakini aliahidi kulifuatilia suala hilo kwa afisa wanyamapori wa Wilaya ili kupata uhakika na takwimu halisi.
Mtendaji wa kijiji cha Murito Joseph Patrick Ntora na mweyekiti wa kitongoji cha Kengoka wamethibitisha kuwapo kwa matukio hayo huku akisema kwa miezi miwili aliokaa katika ofisi hiyo ya kijiji hicho hakuna takwimu zozote kuhusiana na matukio hayo ingawa amekiri kuwa taarifa zipo ingawa sio rasmi huku akiirushia lawama idara ya maliasili kwa kushindwa kuwathibiti wanyama hao wasiwamalizie wananchi mifugo.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Kengoka Mwita Chacha amesema kuwa tatizo kubwa liko kwenye kitongoji chake na kile cha Nyabiherero na tayari mkazi mmoja wa kitongoji chake alikwisha uawa na mamba wakati anaoga mto Mara ambao ndio wananywesha ng’ombe na kuoga.
Amemtaja aliyeuawa kwa mamba kuwa ni kijana wa Kichele Mwita Kichele na baadhi waliojeruhiwa ni Gesabo Garya aliyeumwa mguu wa kulia na mamba huku Bhoke Marwa Sarya akijeruhiwa na miguu na sasa amelazwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Mara kwa matibabu.
Aidha fisi wa ajabu anayeng’oa uzio wa zizi na kuchukua ndama, mbuzi na kondoo kandoo 32 wameliwa na sasa amewafanya wakazi wa vitongoji hivyo kuwa na mawazo ya kuacha ufugaji ingawa ndio wanaoutegemea katika shughuli zao za kuendeshea maisha.
Mkazi wa kitongozi hicho Ephraim Yohana amesema msaada wao wanautegemea kutoka serikalini kwa kuwa wao wakiamua kuwashughulikia wanyama hao hawana kibali cha kufanya hivyo.