UHABA WA MAJI YA BOMBA UNAVYOWATESA WANANCHI TARIME.
AKICHOTA MAJI. |
UHABA WA MAJI YA BOMBA
UNAVYOWATESA WANANCHI TARIME.
MAKALA.
BINADAMU akiuguwa na
kupungukiwa maji mwilini shartiataongezewa maji na iwapo maji yakikosa mwilini
basi Bindamu huyo anaweza kupoteza maisha,vivyohivyo katika matumizi mbalimbali
ya Binadamu yanategemea maji,Maji ni Uhai,ili upike Chakula,uoge, ufue
nguo na shughuli zingine lazima uwe na maji,maji ndiyo mkombozi wa kila kitu.
Licha ya maji kuwa ni
kitu muhimu sana katika maisha ya watu hata hivyo bado ni changamoto kubwa
kwakuwa ni haba hayatosherezi mahitaji ya wananchi wanaoishi ndani ya
Halmashauri ya Mji Tarime Mkoani Mara jambo ambalo limekuwa ni kero .
Wananchi wengi Wilayani
Tarime wamekuwa wakitumia maji ya visima ambavyo vingi vimechimbwa na
wananchi wenyewe ,hata hivyo nyakati za kiangazi visima hivyo ukauka na
wananchi kulazimika kutembea mwendo mrefu zaidi ya kilomita 5 kutafuta maji
mtoni.
Kwa kutambua kero hiyo
Serikali ikaamua kuanzisha mradi wa maji ya bomba kutoka kwenye chanzo cha
maji cha asiri cha Nyandrumo kata ya Kitare Wilayani hapa ili wananchi
wasitegemee tu maji ya visima na badala yake wapate maji ya bomba kama njia ya
kupunguza kero ya maji.
Pamoja na jituihada hizo
za Serikali bado hazijazaa matunda kutokana na chanzo hicho cha maji kulemewa
kwakuwa wahitaji wa maji ni wengi,lakini pia mambomba yanayopokea maji kutoka
kwenye chanzo hicho yamezeeka ni ya zamani tangu uanzishwe mradi huo wa maji ya
bomba mwaka 1974 mabomba hayajawahi kubadilishwa yamezeeka na yamepasuka hivyo
kusababisha maji mengi kupotea kabla ya kufika kwa watumiaji.
Je ni kwanamna gani
wananchi wanavyopata shida ya maji ya bomba katika Mji wa Tarime?
Rhoda Wambura
mkazi wa Rebu mjini Tarime anasema kuwa kwakuwa yeye hana kisima mamlaka
ya maji safi na taka ikamuunganishia huduma ya maji ya bomba,licha yakulipa
bili ya maji kila mwezi bado anapata shida ya maji hasa wakati wa kiangazi
ndiyo kabisaaa uyapata kwa wiki mara mbili hadi mara moja.
“Mtaa wetu wa Rebu senta
ndiko kuliko na tenki la maji lakini unashida sana ya maji uhakika wa maji
unakuwepo wakati wa mvua tu tofauti na hapo maji utayapata kwa wiki mara moja
,tena wakati wa kiangazi unaweza kumaliza wiki mbili hujaona maji kuna
mitaa ina maji kila siku lakini mitaa mingine haipati maji mwisho wa mwezi
unadaiwa bili kwakweli tunaiomba Serikali itatue kero ya maji katika baadhi ya
mitaa mji wa Tarime na tufungiwe mita za maji ili tuwe tunalipa
kile tunachokitumia”anasema Wambura.
Ghat Marwa Mkazi wa
sabasaba anasema”Maji yenyewe unayalipia bili lakini nimachafu mithiri ya
tope huwezi kufulia nguo nyeupe mi nashangaa tunalipa bili kila mwisho wa mwezi
kama mimi huwa nalipa bili kati ya 5,000 hadi 10,000 kwa mwezi lakini maji
hayawekewi dawa ili yawe meupe inabidi uyaache uwende kuchota kisimani ambayo
ni safi”anasema.
John Simoni Mkazi wa
Ronsoti anasema kuwa sababu ya kuwepo kwa shida ya maji inatokana na kuwepo kwa
tenki moja la maji tena dogo sana ukilinganisha na idadi ya watu katika
maeneo,tenki lipo Mtaa wa Rebu ambalo usambaza maji kwenye mitaa
mingi na wahitaji ni wengi na hivyo maji kutotoshereza na kusababisha
kuwepo kwa kero ya uhaba wa maji mjini Tarime.
Vitals Nyang’ure ni
mlizi kwenye chanzo cha maji cha asiri ambacho maji yote ya bomba wanayoyatumia
wananchi ndani ya Halmashauri ya mji yanatoka kwenye chanzo hicho anasema
chanzo cha maji Nyanduruma kina kabiliwa na changamoto kadha wa kadha.
Nyang’ure anasema kuwa
mabomba yaliyowekwa kwenye chanzo cha maji ambayo upokea maji na kusambaza
kwenye matenki ya maji ni ya zamani na ni ya saizi ndogo 6
yameshazeeka hivyo yanalemewa na wakati mwingine uziba kutokana na
kujaa tope nakwamba yanapaswa kubadilishwa na kuwekwa mapya .
Anaongeza kuwa Chanzo
hicho kina magugu maji ambayo yanatakiwa yaondolewe lakini pia kuna haja
yakuweka karavati kwenye barabara usawa wa chanzo cha maji kwakuwa wakati wa
mvua maji yanayotoka kwa wakazi wa Kenyamanyori kisha utililika na
kuingia kwenye chanzo hicho na kusababisha maji kuwa machafu .
Meneja wa Maji safi na
Usafi wa Mazingira anakiri kuwepo kwa changamoto katika huduma ya maji Tarime
Mjini.
Faustine Makoka ni
Meneja wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Tarime anasema
kuwa kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 Halmashauri ya Mji wa Tarime kwa
sasa inakadiriwa kuwa na wakazi wapatao elfu 84,546 na inajumla ya kata 8 na kati
ya hizo ni kata 4 pekee zinazopata maji ya Bomba tena ni baadhi ya maeneo.
Anazitaja kata
zinazopata huduma ya maji ni Turwa,Sabasaba,Bomani na
Nyamisangura na nimaeneo machache yanayopata maji ambapo jumla ya
kata zote 4 zina jumla ya wananchi wapatao elfu 41,076 na wanachi
22,592 ndiyo wanaopata maji sawa na asilimia 55% huku idadi ya
wateja wa maji ikiwa ni elfu 1,425.
Anasema kuwa idadi
ya watu katika Mji wa Tarime imekuwa ikiongezeka siku hadi siku kutokana
na kuwepo kwa watumishi wa maeneo jirani kama vile Rorya,sirari,Musoma na Mgodi
wa Nyamongo pia hali nzuri ya Maisha na kuwepo kwa fursa mbalimbali za
kibiashara ni sababu ya ongezeko na kusababisha uhaba wa maji.
Ofisa huyo wa Mamlaka ya
Maji anakiri kupokea malalamiko hayo”anasema ni kweli katika maeneo hayo kuna
kero ya hupatikaji wa maji kutokana na eneo hilo kuwa juu,hivyo maji
yanapofunguliwa kwenye tenki huwa na tabia ya kukimbilia maeneo ya mjini ambako
ni sehemu ya muteremuko mkali sana” anasema Makoka.
Anaongeza”Hali hiyo
usababisha maji kushindwa kupanda maeneo yenye mpando ikiwepo
Rebu senta ,watu wanaoishi
maeneo ya mpando upata maji hadi pale wananchi wanaoishi kwenye mitelemko
wanapochota maji wakaridhika au upata maji nyakati za mvua ambapo matumizi ya
maji ya bomba kwa wananchi huwa ni kidogo ndo maji yanaweza kupanda
juu maeneo hayo ya Rebu senta.
Makoka anasema kuwa kwa
kulitambua tatizo hilo katika eneo la Rebu senta tayari wamekwisha nunua vifaa
vya kuweza kutatua tatizo hilo ikiwa ni pamoja na kufunga sluice valve
kwa lengo la kusambaza maji kwa mgao kwa masaa 8 kwa siku .
Aeleza sababu
ya maji kuwa machafu.
Meneja huyo wa Maji
anasema kuwa ni kweli kuna wakati maji huwa machafu hasa wakati wa mvua ambapo
maji utililika kutoka kwenye makazi ya watu na kuingia kwenye chanzo cha maji
lakini pia kutokuwepo kwa mtambo wa kutibu maji(Water Treatment Plant) katika
Mamlaka ya Maji Tarime ni tatizo kubwa .
“Matenki yanazidiwa
sana kwani tuna matenki manne(4) tu yenye jumla ya uwezo wa kuhifadhi
lita za maji 680,000 na uzalishaji wetu wa maji ni lita 1,118 kwa
siku sawa na asilimia 32% tu ya uzalishaji wakati mahitaji ya maji katika
mji wa Tarime ni lita 3,500 kwa siku,Hatuna mtambo wa kutibu maji(Water
Treatment Plant) kwa usahihi huwa kuna hatua kadhaa za kutibu maji kabla
hayajaenda kwa watumiaji”anasema.
Anaongeza”unatakiwa
kuweka dawa ili maji yajichanganye vizuri baada ya kuwa tope limechujwa
na limetolewa kwenye maji kisha dawa ya kusafisha maji inawekwa ili
maji yawe safi na salama baada ya hapo yanakwenda kwenye tenki la kuhifadhia
maji safi(Safe Water Tank) tayari kwenda kwa watumiaji. lakini kwa hapa Tarime
hatuna mtambo wa kutibu maji(Water Treatment Plant) hivyo tunatibu maji
haya kienyeji(manual treatment) tu tunaweka dawa kwenye Tenki wakati
huohuo maji mengine yanaingia kwenye tenki inakuwa ni shida na kusababisha maji
yote yasipate dawa ya kutosha na hata kuwa masafi”anasema.
Makoka anazidi kusema”
kwa utaratibu huo unakuta unaweka dawa wakati huohuo maji mengine yanaingia
tenkini yanachanganyikana kutokana mfumo wetu wa usambazaji wa maji ulivyo,Maji
yanaingia kwenye Matenki na kutoka kwenda kwa watumiaji moja kwa moja (direct
pumping) na huwezi kuyafunga kwa mda mrefu kwani Mahitaji ya Maji katika
Mji huu ni makubwa sana na hata ukifunga tenki ili uweke dawa maji hayo
hayatawatosheleza wananchi kwakuwa manteki ni madogo maji yatakayokuwa na
dawa ni kiasi kidogo na utakapoyafungua maji huingia kwa kasi na
kuchanganyikana yenye dawa na yasiyo na dawa”anasema
Makoka anasema kuwa
kwa wale walio na mita ulipa bili/ankara zao kulingana na matumizi yao wenyewe
ambapo idadi ya wateja wenye mita/dira za maji ni 610 kati ya wateja
1,425 sawa na asilimia 43% lakini wasiokuwa na mita wao malipo yao ni ya
kukadilia(Flat Rate) ya sh.5,500 hata kama mteja alitumia maji mengi au laa!
Jambo ambalo kwa upande mwingine mteja au Mamlaka ya Maji Tarime uingia hasara
kubwa.
“Kwa uniti moja
ambayo ni sawa na lita 1,000 ni Tshs 540 na tozo ya huduma
1,000(service charge) kwa wateja wa matumizi ya Majumbani tu,na mteja mpya kwa
sasa anayetaka kuunganishiwa Maji gharama za kununua mita inakuwa ni sehemu
moja wapo kwenye gharama anazotakiwa kulipa ili aunganishiwe maji,huu ni
utaratibu wa kawaida kabisa kwa mamlaka ukiwa na lengo la kuwafanya wateja wetu
wote kufungiwa dira za maji/mita ili waweze kulipa bill/ankara zao kulingana na
kiasi cha maji walichokitumia kwa mwezi anasema kuwa pamoja na changamoto
hizo hadi mwezi April 2016 wananchi na Taasisi mbalimbali za Serikali
zinadaiwa bili za maji jumla ya madeni yote ni Tshs milioni 24,268,670
Serikali yatakiwa kutoa
fedha kumaliza kero ya maji katika Mji wa Tarime.
Makoka anasema Serikali
ikitoa fedha zitasaidia kuondoa kero ya maji kwakuwa mikakati ya mamlaka ya
maji Tarime ni kutarajia kutoa maji Ziwa Victoria kwani ndo chanzo pekee
cha Maji cha kudumu,kutoa Maji ziwa victoria kutasaidia upatikanaji wa maji ya
kutosha katika mji wa Tarime pamoja na baadhi ya vijiji vilivyoko katika wilaya
jirani kama vile wilaya ya Rorya na wilaya ya Tarime ambapo mradi huu utapita
katika vijiji hivyo kama serikali itaamua kutekeleza mradi huu muhimu kwa
wananchi utawanufaisha.
Hata hivyo Meneja huyo
anasema kuwa Serikali ilikuwa imeandaa mpango wa mda mrefu wa kujenga mradi wa
maji Tarime mjini kwa kutumia chanzo cha maji kutoka mto Mori kwa gharama ya
Tsh Bilioni 17 lakini kwa sasa chanzo hicho cha maji mto mori hakifai tena
kwani wakati wa kiangazi maji yake yanapungua kwa kiasi kikubwa ,na maji yake
ni machafu .
Anasema hali
upelekea gharama kubwa kutibu maji ili yawe safi na salama na uwezo wake
wa maji ni kdogo sana kulinganisha na mahitaji ya maji ya sasa kwa wananchi wa
mji wa Tarime ambayo ni takribani lita 3,500.kwa siku.
Hata hivyo Anaiomba
Wizara ya Maji kuongeza fedha zingine pamoja na kiasi hicho kilichokuwa
kimepangwa kwa ajili ya chanzo cha mto Mori Bilioni 17 ili kufanikisha maji
kutoka Ziwa Victoria nasiyo mto Mori kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali mwaka
2010.