DC TARIME AWATAKA WATAALAMU WA HALMASHURI KUBAINISHA FURSA ZILIZOPO.
DC TARIME AWATAKA WATAALAMU WA
HALMASHURI KUBAINISHA FURSA ZILIZOPO.
Mkuu wa Wilaya
ya Tarime Glorius Luoga amewataka wataalamu
wa Halmashauri zote mbili Halmashauri ya Mji wa Tarime na Halmashauri ya Wilaya
ya Tarime kukaa pamoja na kubainisha fursa zilizopo kwa ajili ya uzalishaji wa
malighafi ili kuwapatia fursa wawekezaji kutoka maeneo mbalimbali kwa lengo la
kuinua uchumi ikiwa ni pamoja na kupatikana kwa ajira kwa vijana kutokana na
fursa hizo ikiwemo kilimo cha Miwa,Ufugaji wa samaki katika Mto Mara na Bihashara.
Hayo
yamebainishwa katika kikao cha Baraza la wafanyabihashara kilichofanyika katika
Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya kwa
kushirikisha Halmashauri zote mbili huku mwenyekiti wa kikao hicho akiwa mkuu
wa Wilaya ya Tarime Glorius Luoga.
Luoga
alisema kuwa kulingana na fursa zilizopo katika wilaya ya Tarime ukiwemo mto
mara wataalamu hao kutoka katika Halmasauri zote mbili hawana budi kukaa kwa
pamoja na kubainisha fursa hizo na kuanza kuzitangaza mara moja ili kuwavutia
wawekezaji ili waweze kuwekeza kwa lengo la kuinuchumi na kuongeza vipato
katika Halmashauri hzo.
Mkwa mfano
tuna bonde la mto mara watu wanaweza kufuga samaki pia hata kilimo cha miwa kwa
sasa ni dilibaada yam h rais magufuli kupiga marufuku sukari kutoka nje ya Nchi
alisema Luoga.
Hata hivyo Mkuu
wa wilaya alisema kuwa maeneo yatakayotengwa kwa ajili ya ywekezaji wahakikise
hayana mikwazo vyovyote na pamoja na migogoro ili wawekezaji wasije kusumbuliwa
na wananchi.
Mordikae
Moset ambaye alikuwa mjumbe katika kikao hicho alisema kuwa mbali na Watanzania
kujikwamua kupitia kilimo lakini kanda
ya ziwa hakuna mahabara ya kupima udongo ili kubaini udongo mzuri kulingana na
aina ya kilimo ili wakulima waweze kuongeza uzalishaji.
“Tanzania
ndiyo maana tuko nyuma nchi jirani ya Kenya wakulima kabla ya kuanza kilimo
wanaenda kwenye mahabara nakupima udongo na kubaini kuwa udongo huo unastahili
kilimo gani lakini sisi hata kanda ya ziwa yote hatuna maabara ya kupimia
udongo tunalima mwisho wake mazao yote yanaharibika” alisema Moset
Awali Afisa
bihashara katika Halmashauri ya mji wa Tarime Charles Launces amebainisha
baadhi ya fursa zilizopo katika Wilaya Ya Tarime ikiwa ni pamoja na,Uzalishaji
wa madini , Ujenzi wa kiwanda cha kuchakata kahawa kavu na Mbivu, ujenzi wa
kiwanda cha kutengeneza Biskuti, ujenzi
wa kiwanda cha utengenezaji wa Mvinyo kutokana na Ndizi , ukamilishaji wa
kiwanja cha ndege Magena ,ujenzi wa
uwanja wa mpira katika Halmashauri ya mji wa Tarime,mkoani Mara.
…