JERA MIAKA 30 KWA KUJERUHI KWA SHOKA,MIAKA 5 KWA KUJERUHI SEHEMU ZA SIRI.
JERA MIAKA 30 KWA KUJERUHI KWA
SHOKA,MIAKA 5 KWA KUJERUHI SEHEMU ZA SIRI.
MAHAKAMA ya
Wilaya ya Tarime imemuhukumu kwenda jera miaka (30) mtu mmoja anayejulikana kwa
jina la Nicolous Makongoro mkazi wa kijiji cha Omoche kata ya Nyamtinga Wilayani
Rorya mkoani Mara. kwa kosa la
unyang’anyi wa kutumia silaha
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu mfawidhi
Mahakama ya Wilaya ya Tarime Martha Mpaze
na kwamba kwa upande wa mashitaka umethibitisha kosa pasipo na shaka.
Awali
Mwendesha mashitaka wa Jeshi la Polisi George Lutonja alisema kuwa mshitakiwa mwenye
kesi No.388//2015 mnamo 1,juni,2015 saa 12 asubuhi kijiji cha Kyariko
mshitakiwa alimjeruhi kwa shoka mgongoni Jumanne Siagi na kukimbia
kusipojulikana.
Lutonjs
alisema kuwa mshitakiwa pia alimwibia simu 2 zenye thamani ya laki laki 2 na
Nyaraka zenye thamani ya laki tatu ambapo 15,7,2015 alikamatwa na polisi na
kuhojiwa na 16,7,2015 alifikishwa mahakamani na upande wa mashitaka ulikuwa na
mashahidi 5 waliothibitisha makosa wa upande wa mshitakiwa hakuwa na shahidi.
Wakati huohuo,MAHAKAMA hiyo imemuhukumu kifungo cha
miaka 5 jera Masco Chacha (29)mkazi wa
kijiji cha Kemange kata ya Bomani kwa kosa la kumjeruhi sehemu za siri Marwa Msome(52) mkazi wa kijiji cha Ntagacha
Kata ya Ganyange Wilayani humo.
Hukumu hiyo
ilitolewa na Hakimu mkazi wa mahakama ya Wilaya ya Tarime Amon Kahimba ambapo
upande wa mashtaka umethibitisha kosa pasipo na shaka.
Awali
mwendesha mashtaka wa Polisi Inspecta Abel Kazeni alisema mshitakiwa mwenye
kesi No.326/2015 mnamo 13/juni/2015 majira ya saa 11 jioni kijiji cha Nyakarima
mshitakiwa alimjeruhi Marwa Msome sehemu za siri na kumsababishia maumivu
makali.
Kazeni
alisema kuwa Mshitakiwa alikamatwa 15,juni ,2015 na kufikishwa polisi kwa
mahojiano na 18,juni ,2015 alifikishwa mahakamani.
Aidha kwa upande
wa mashitaka ulikuwa na mashahidi 4,mshitakiwa hakuwa na shahidi na wakati wa
kujitetea aliomba apunguziwe adhabu kwakuwa ni mgonjwa na anafamilia.