MWENYEKITI WA HALMASHAURI ATUMBUA WATENDAJI TISA WAKIWEMO WALIMU NA WATENDAJI WA KATA.
PICHA YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME AMBAYE PIA NI DIWANI WA KATA YA NYAMWAGA (CHADEMA) ALIPOKUWA AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE. |
Akiongea na waandishi
wa habari ofisini kwake mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Moses
Matiko Misiwa ambaye pia ni dwani wa kata ya Nyamwaga amesema kuwa
amewasimamisha watenadji wa kata wanne ambao ni aliyekuwa mtendaji wa kata ya
Kemambo Stiven Cheche ambapo kwa sasa
alikuwa amehamishiwa kata ya Sirari,
Ibraimu Makuli alikuwa amehamishiwa kata ya Mwema, Kata ya Nyamwaga Hezron
Makaranga, na Pendo Aizak kata ya Binagi
ambaye ameshindwa kusimamaia fedha za ujenzi wa ujenzi wa zahanati ya
kijiji cha Nyamwigula .
Walimu wakuu
katika shule za sekondari waliosimamishwa ni Mwalimu mkuu katika shule ya sekondari KemamboMwl Daniel Magige,Shule
ya sekondari Inchugu Samwel Mahisa, Nyamwaga Sekondari Mwita Nyambacha akiwemo
mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Nyamongo kwa udanganyifu wa idadi ya
wanafunzi ili kupewa fedha nyingi jambo ambalo ni kinyume cha sheria kulingana
na utumishi wa umma.
“Huyu
mwalimu mkuum katika shule ya sekondari Nyamongo aliweza kudanganya Hazina
pamoja na serikali kwa ujumla kwa maana ya Halmashauri baada ya kufuta micango
na tunapeleka fedha katika shule za sekondari kulingana na takwimu ya wanafunzi
hivyo alifoji wanafunzi kuwa shule hiyo inajumla ya wanafunzi karibia Elfu
mbili huku idadi ikiwa ni wanafunzi wasiozidi miasita ivyo tumeomba hazina
watupe akaunti ili aweze kurudisha fedha hizo na mamlaka huska watamuchulia
hatua kali kuhusu nidhamau lakini kwa sasa tumemusimamisha ili uchunguzi
ufanyike” alisema Misiwa.
Mwenyekiti
huyo alisem kuwa wamehamua kuwasimamaisha kazi watendaji hao baada ya kuwatilia
shaka ili wapishe uchunguzi na pale watakapo bainika kuwa wamefanya ubadhilifu
huo hatua kali zitachukuliwa kulinga na kanuni na tararibu za utumishi wa umma.
Baada ya ubadhilifu
huo wa fedha za serikali ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watendaji wa
serikali umekuwa ukikwamisha maendeleo ya wanachi na wanachi kuendelea kulaumu
serikali hivyo mwenyekiti huyo alitumia
nafasi hiyo kutoa wito kwa watumishi wa serikali kuendelea kufuata misingi na
taratibu za utumishi wa uma na kudai kuwa katika uongozi wake yuko tayari
kufanya kazi na watu wachache wenyemaadili ya kazi kwa lengo la kuletea wanchi
maendeleo.
Nadhani
watumishi wa serikali wanajua kasi ya hawamu ya Tano niko radhi kubaki na
mtumishi mmoja mwenye maadili kwa ajili ya kutunza rasilimali za nchi kulingana
na katiba inavyosema alisema Matiko