MADIWANI WAPINGA TOZO YA KODI YA MAJENGO HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME
PICH AYA MADIWANI WA KATA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME MKOANI MARA. |
Madiwani wa
Halmashauri ya Wilaya ya Tarime wamekataa Tozo ya majengo ambayo imepangwa kwa
mujibu wa sheria ili kuweza kuziongezea mapato Halmashauri za Wilaya na Miji
hapa Nchini kwa kudai kudai kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime inavyanzo vya
kutosha kwa ajili ya kuendesha Halmashauri hiyo ukiwemo Mgodi wa Uchimbaji wa
dhahabu ACACIA, Mpaka wa Kenya na Tanzania Sirari pamoja na Mbuga ya Wanyama
Serengeti.
Hayo
yamebainiswa na madiwani hao katika balaza la kawaida la madiwani hao
lililofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Petros Itala ni
diwani wa kata ya Mwema akiongea mbele ya madiwani hao alisem akuwa kodi hiyo ya majengo imeanza kutozwa kwa
wanachi kabla ya kutungwa kwa sheria ndogondogo za Halmashauri na kuletwa kwa
madiwani ili ziweze kupitishwa ili zoezi hilo liweze kufanyika mara moja.
Baada ya
kutolewa kwa hoja hiyo mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni mwenyekiti wa
halamashauri ya wilaya ya Tarime Moses Matiki Misiwa aliweza kuwauliza madiwani
hao kuwa tozo hiyo iendelee kutozwa au waachane nayo ndipo madiwani wote
waliunga mkono hoja ya hiyo na kuamua kupinga suala hilo.
Zabroni
Mrimi ni katibu wa Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini John Heche amesema kuwa kuwa kwa niaba ya mbunge amewaunga mkono
madiwani hao kuhusiana na kupingwa kwa tozo ya majengo huku akisema kuwa
serikali imeanza kutekeleza suala hilo kabla ya kupimwa kwa ardhi ili
kuondokana na maigogoro ya ardhi.
Aidha katibu
huyo alisema kuwa kulingana na vyanzo vya mapato vilivyomo ndani ya Halmashauri
tayari vinatosha kuendesha Halmashauri hiyo hiyo wataendelea kutoa elimu kwa
wanachi baada ya vyanzo vya mapato ukiwemo Mgodi, Mbuga ya Wanyama na mpaka wa
Sirari kushindwa kuleta mapato
wataruhusu hoja hiyo lakini siyo kwa wakati huu.
Athuman
Akalama ni mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime alisema kuwa endapo
madiwani hao watakataa kutozwa kwa tozo hizo kwani agizo hilo limetolewa Nchi
nzima watakuwa wamekika utaratibu wa sheria nakuwaomba madiwani hao badala ya
kukataa waweze kurekebisha baadhi ya vifungu kwa lengo la kutimiza lengo ili
kukusanya mapato.
Kwa upande
wake katibu tawala Halamashauri ya wilaya ya Tarime John Marwa alisesema kuwa maendeleo ya wanachi
yanafanyika kutokana na kodi za wanchi hivyo jambo hilo la madiwani kupinga
tozo hilo limemushangazanakusema kuwa kipindi madiwani wakati wa kampeni
walihaidi kuletea wanchi maendeleo hivyo hawakuwa na sababu ya kupinga bali
wangeboresha kwa lengo la kupata pesa za kutekeleza miradi waliyowahaidi
wanachi hao huku Halmashauri ikisimamia vyema fedha hizo.