MAHAMAKA YAMUHUKUMU MAISHA
MAHAMAKA YAMUHUKUMU MAISHA
MAHAKAMA ya hakimu mkazi mfawidhi Wilaya ya Tarime mkoani Mara
imemuhukumu kifungo cha maisha Mwita Charles (20) mkazi wa Kata ya Bomani Wilayani
humo kwa kosa la kumbaka mtoto wenye
umri wa miaka 5 mkazi wa kata ya Bomani
jina limeifadhiwa .
Hakimu mkazi
mfawidhi mahakama ya Wilaya ya Tarime Amon Kahimba kipindi akitoa hukumu hiyo alisema kuwa upande wa mashitaka umethibitisha bila kuacha
shaka nakwamba mshitakiwa amehukumiwa
kifungo cha maisha jera ili liwe
fundisho kwa watu wengine.
Awali
Mwendesha mashitaka inspecta wa Polisi Abel Kazeni aliieleza mahakama kuwa
mshitakiwa huyo alitenda kosa hlio mnamo juni
30,2015 huku akisema kuwa
mshitakiwa huyo anakabiliwa na kesi namba CC.353/2015.
Aidha
Mwendesha mashitaka aliambia mahakama kuwa mshitakiwa huyo alikuwa akipanga
nyumba moja na wazazi wa mtoto huyo kata ya Bomani Wilayani Tarime mkoani Mara
nakusema kua kitendo hicho cha unyama kilfanyika majira ya saa 11 jioni na ndipo
alishikiwa na jeshi la polisi na kufikishwa
na mahakamani julai 3/2015.
Aidha kwa upande wa mashitaka mashaidi walikuwa watano ambao ni Mama mzazi
wa mtoto huyo, Jirani ,Mtoto mwenyewe ambaye ni mhanga wa tukio hili la
kinyama,Polisi pamoja na Daktari kwa upande wa mshitakiwa hakuwa na shahidi
yeyote, baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo mbele ya mahakama mshitakiwa huyo aliomba mahakama
kumunpunguzia mihaka huku akidai kuwa na familia ya mwaanmke mmoja na mtoto
mmoja.
Hata hivyo
imesemekana kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akimlagai mtoto huyo kwa pipi na
kumufanyia vitendo hivyo vya ukatili na ndipo mama mzazi wa mtoto huyo alitaka
kumwogesha na kusikia harufu na badae kugundua kuwa amekuwa akifanyiwa vitendo
hivyo.
Daktari
alidhibitisha tikio hilo nakusema kuwa mtoto huyo amekuwa akibakwa na
kusababishiwa magonjwa ya zinaa.
Jambo leo imweza kuongea na baadhi ya wanachi
wakazungumzia juu ya kutolewa kwa hukumu hiyo huku wakilaani vikali vitendo vya
ukatili ambavyo vinawakumba watoto wa kike wilayani Tarime Mkoani Mara.