MKUU WA WILAYA YA TARIME ATOA SIKU KUMI KWA WAMILIKI WA MAJENGO,VIWANDA NA SHELI ZA MAFUTA KULIPIA TOZO.
PICHA YA MKUU WA WILAYA YA TARIME GLORIUS LUOGA AKITOA AGIZO HILO MBELE YA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE. |
MKUU WA WILAYA YA TARIME ATOA SIKU
KUMI KWA WAMILIKI WA MAJENGO,VIWANDA NA SHELI ZA MAFUTA KULIPIA TOZO.
Mkuu wa
Wilaya ya Tarime Glorius Luoga ametoa siku kumi kwa wamiliki wote wa majengo ya
bihashara,makazi , viwanda sheli za Mafuta Tanesco,Benki,Nyumaba za kulala
wageni na TTCL katika Halmashauri ya mji
wa Tarime kuhakikisha wanalipa tozo ya majengo kabla ya kufikishwa mahakamani.
Akiongea na
waandishi wa habari ofisini kwake mkuu wa wilaya huyo alisema kuwa kwa mamlaka
aliyopewa na kwa mujibu wa sheria ya
Tawala za mikoa Na19 ya mwaka 1997 kama ilivyofanyiwa marekebisho ya mwaka 2002 na kwa mujibu wa sheria ndogo za kodi ya
majengo za Halmashauri ya mji wa Tarime za mwaka 2015 wamiliki wa majengo hayo
hawana budi kulipia tozo hizo.
Aidha Mkuu
wa Wilaya huyo alisema kuwa
watakaoendelea kukaidi amri hiyo watalazimika kulipa kulipa kodi hiyo pamoja na
faininya asilimia 50 ya deni lote au kukamatwa na kufikishwa mahakamani au
vyote kwa wakati mmoja.
“Tuliweza
kutoa elimu ya kutosha juu ya umhimu wa kulipa tozo hizo pia wananchi na
wamiliki wa majengo, viwanda, sheli walipe kupitia akaunti ya Halmashauri Na
304100053254 NMB Tawi la Tarime na kupeleka na badae kwenda ofisi za
Halmashauri kupewa risti” alisema Mkuu wa Wilaya.
Hata hivyo Luoga
amewaagiza jeshili la Polisi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Tarime,
Maofisa Tarafa na Watendaji wa kata kusimamia na kutekeleza amri hiyo alali
huku akisema kuwa Afisa yeyote atakayeshindwa kusimama hana kazi.
“Nimetoa
amri hii alali ofisa wa serikali atakayeshindwa kutekeleza na kusimami hana
kazi tena” alisema Luoga.
Hata hivyo
mkuu wa wilaya ya Trime amefafanua juu ya viwango vya tuzo hizo kuwa ni Eneo
dogo makzi ni shilingi 10,000 Biashara15,000 Makazi na Biashara shilingi 20,000
, Eneo la kati makazi shilingi 15,000
Biashara 20,000 Makazi na Bishara
shilingi 25,000, Eneo kubwa Makazi shilingi20,000 Biashara 25,000 JMakazi na
Biashara 30,000 kiwanda shilingi 400,000 Ghala shilingi 200,000 Nyumba kubwa ya Biashara shilingi 50,000
Nyumba kubwa ya Bishara na Makazi 80,000
Gholofa ya Makazi shilingi 100,000 pamoja na Gholofa ya Biashara
shilingi 100,000.
Hata hivyo
mkuu wa wilaya amezitaja Taasisi mfano Banki kuwa zinalipia shilingi150,000 kwa
mwaka TTCL50,000 POSTA 50,000 Vituo vya mafuta shilingi 100,000 Tanesco
shilingi100,000 na Nyumba za kulala wageni shulingi50,000.
Halamsauri
ya mji wa Tarime yenye mitaa 81 mpaka sasa inakadiliwa kuwa na majengo Elfu
moja na Mianane