CHADEMA WALAANI SERIKALI YA TANO KUNYIMA UHURU VYOMBO VYA HABARI

PICHA YA KATIBU WA CHADEMA MKOA WA MARA MWL CHACHA HECHE KUSHOTO NI KATIBU WA CHA HICHO WILAYA YA TARIME THOBIA GHATI WAKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUNYIMA UHURU VYOMBO VYA HABARI.




Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kupitia katibu wake Mkoani Mara Mwl Chacha Heche kimesema kuwa haikitakubali utaratibu wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushindwa kuonesha Bunge hilo  ikiwa ni pamoja na kuendelea kunyima uhuru vyombo vya habari huku wakiitaka serikali ya hawamu ya Tano kuondokana na kuingilia kati  Utendaji wa mhimili wa wanchi ambao ni  Wabunge ili wanachi waendelee kupta taarifa za ubunge ili waweze kuwahiji wabunge wao pale watakapokiuka kutetea haki zao. 
 
Kauli hiyo imetolewa na katibu wa Chama hicho nazi ya Mkoa Mwl Chacha Heche kipindi akiongea na waandishi wa habari ofosini kwake ambapo alisema kuwa kama chama wameweza kufanya tafiti nakuona kuwa endapo serikali ya hawamu ya tano inaendelea na suala la utumbuaji wa majipu lakini suala la kunyima uhuru vyombo vya habari ni jipu kubwa hivyo Rais magufuli hana budi kuliona jipu hilo na kulitumbua mapema ili kuwapa wanchi haki yao ya msingi ya kupata habari.

Chacha aliongeza kuwa chama cha Demokrasia kimeitaka serikali ya Chama cha mapinduzi kuingilia  utendaji wa mhimili wanachi kwa maana ya Bunge ili  huku akisema kuwa Waziri mwenye dhamana Waziri wa Habari,Utamaduni, sanaa na na Michezo  ,Nape Nnauye ameshundwa kuachana na ukada wa chama cha mapinduzi na kuwa mtumishi wa watanzania wote.

Hata hivyo katibu huyo aliitaka serikali kufungua  bihashra za mipakani  kwani  kitendo hicho kinasababisha wanchi kuendelea kuwa maskini uku serikali ikitakiwa kuendeleza mfumo mzuri wa kuelimisha wanchi juu ya ulipaji wa kodi  ili kuongoze uchumi.

Kwa upande wake katibu wa madiwani kupitia Chama Cha Demokrasia ma Maendeleo CHADEMA  Halamshauri ya wilaya ya Tarime ambaye pia ni diwani wa viti maalumu  Veronica Sando amesema kuwa jambo la kunyima uhuru wa vyombo vya habari wanazidi kulaani vikali.

Suala hili la serikali kunyima vyombo vya habari ni kuzidi kuacha wanachi gizani pia tunaendelea kumushangaa waziri mkuu ambaye amewasilisha Taarifa ya serikali gizani mpaka sasa wanchi hawajui nchi inatoka wapi na kwenda wapi alisema Veronica.

Naye Diwani wa Nyarokoba Bisendo Marwa alisema kuwa pale bunge linaporushwa uwapa fursa wanachi kumukumbusha mbunge wao pale anaposahau kuwasilisha baadhi ya kero ambazo zinawakumba wanchi hao

Powered by Blogger.