DC RORYA AINGILIA KATI MGOGORO KUWAKOMBOA WANACHI.
DC RORYA AINGILIA KATI MGOGORO KUWAKOMBOA WANACHI.
Mkuu
wa Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Felix Lyaniva ameingilia kati mgogoro wa
uendeshaji wa mradi wa kilimo cha mpunga wa kijiji cha Ochuna uliokuwa
ukiendeshwa na serikali baadaye ukaachwa na kushindwa kufikia malengo yake.
Mradi
huo uliokuwa ukisimamiwa na serikali ulianzishwa mwaka 2000 ilipofika mwana
2010 serikali ilijitoa kutokana na kupelekwa mahakani na watu waliodai eneo la
mradi lilikuwa mali yao na kuonekana kushinda kesi hiyo baada ya
kuunguruma kwa miaka 10 wakidai fidia ya maeneo yao.
Mradi
uliingia mgogoro baada ya watu 11 kwenda mahakama ya wilaya ya myumba, ardhi na
makazi baada ya kushinda kesi ya madai yao katika baraza la ardhi la kata na
kufanikiwa kurudishiwa maeneo hayo ambayo mkuu wa Wilaya aliuita kuwa ulikuwa
mgogoro wa kimaslahi ya watu binafsi.
Baada
ya serikali kujiondoa kwenye mradi huo uliogharimu sh, milioni mia nane
na laki sita, walimiliki wa hekari 120 zilizokuwa kikitumika kwenye mradi
walianza kulima wenyewe na wakikodisha maeneo hayo kwa waliohitaji njia
inayotumika hadi sasa ambapo mkulima anapilia sh, 70,000 kwa hekari moja.
Tangu
mwaka 2010 serikali ilipojitoa kwenye mradi huo, ulipoteza mwelekeo na kuanza
kuzuka kwa mgogoro wa kimaslahi kati ya vikundi vilivyoanzishwa kusimamia mradi
huo ambapo kikundi cha mwanzo kiliondolewa na kuundwa kikundi cha pili
kilichoitwa “Mradi wa umwagiliaji mpunga Ochuna” lakini kikikumbwa na
tatizo la kutokuwa na madaraka halisi kwa kuwa kikundi cha kwanza hakikutaka
kuridhika na hali ya usimamizi wake.
Kutoka
na mgogoro mkuu wa Wilaya aliingilia kati na kuchukua maamuzi kwenye kikao cha
kamati ya ulinzi na usalama wa vijiji viwili vya Nyajage na Ochuna, kwa
kukivunja kikundi kilichopo sasa na kuunda kamati ya kuunda upya kikindu
kitakacho simamia mradi huo (task force) ambayo ameipa siku 14 kumaliza
shughuli ya kuandaa mpango mkakati wa nini kifanyike ili kumaliza tatizo la
usimamizi na wananchi wanufaike na mradi huo.
Lyaniva
alikiri kuzorota kwa mradi na kusema kuwa haujawanufaisha wananchi kama
serikali ilivyoukusudia kwa kuwa kuna mgongano wa kimaslahi,.
“Leo
nimekuja kukutana na sehemu zote mbili ili kuona mgogoro unaisha na skimu
inaendelea kufanya kazi, tumefikia maamuzi mazuri ya kuunda kikindi kingine
kitakachoendesha mradi kwa kanuni na taratibu ili kuunda kikundi hicho tumeunda
taskforce itakayojumuisha wataalamu kutoka halmsahauri , na wananchi na
viongozi wa pande mbili za kijiji cha Ochuna na Nyanjagi” alisema mkuu huyo na
kuongeza
“kwa
hatua hii mgogoro huu utaenda kuisha na ndani ya wiki mbili mambo yote yatakuwa
yameisha na tutawatangazia wananchi kuwa mradi unaanza upya….. lakini kukiwa na
mgawanyo wa usimamizi, miundo mbinu ya maji itasimamiwa na serikali kwa
kushirikiana na kikundi na wananchi ili kuiboresha zaidi na kuleta tija kwao”
alisema Mkuu wa Wilaya alipokuwa akiongea na gazeti hili.
Aliongeza
kuwa lengo lake ni kuona wananchi wanafaidika na sikimu hiyo ili kufikia kaulimbiu
anayoitumia “Rorya bila njaa inawezekana” kwa kuwa sikimu hiyo ni moja na
eneo linaloangaliwa na serikali kuwa litaleta mabadiliko ya kilimo kwa wananchi
wa Rorya.
Mwenyekiti
wa kikundi cha mradi wa umwagiliaji mpung cha Ochuna Daudi Ogo anakili
kutokuwepo na mafanikio tangu serikali ilipoondoa mkono wake kwenye mradi huo.
“Mwanazoni
kulikuwa na mafanikio makubwa lakini kuanzia mwaka 2010 hakuna mafanikio yoyote
kwenye mradi huu na kwenye kikundi maana tumefanya kazi kwa wakati mgumu
kutokana na vurugu la wamiliki wa maeneo... kwa ujio wa mkuu wa Wilaya sasa
tunaona suluhisho utaleta mafanikio” alisema Ogo.
Aliongeza
kuwa kuzorota kwa mradi huo wa kilimo cha umwagiliaji serikali ilichangia kwa
kutokutimiza ahadi kuwafidia wananchi waliotoa maeneo yao kwa miaka 10 lakini
na kuonyesha wasiwasi kuwa ikiwa tena hawatapewa maneo tatizo linaweza
kujirudia tena.
“Wale
wa kijiji cha Nyanjage walitakiwa kufidiwa na serikali ya kijiji cha Nyanjage
na wale wa Ochuna hivyo hivyo lakini kwa miaka 10 walidai na wakawa wanapigwa
chenga tu bila mafamikio ndipo wakaamua kwenda mahakamani… watu tisa
kutoka Ochuna na watu watatu kutoka Nyanjage ndio waliofungua jarada
mahakamani” alisema Ogo.
Kutokana
na mgogoro huo kikundi cha usimamizi kiliathirika kwa kushindwa kufikia malengo
ya uzalishaji wenye tija ili kuwanufaisha wananchi.
“Mitaro
imeziba, maji hayafiki kwenye majaruba, zamani ulikuwa ukiomba maji yanakufikia
kwa wakati lakini baada ya kuondoka serikali miundombinu imeharibika vibaya
njia za kupitishia mifugo zimelimwa, bwawa halina maji ya kutosha kama
ilivyokuwa zamani” alisema Ogo.
Mwenyekiti
wa kikundi cha kukoboa mpunga Okinyi Ojijo alisema kuwa kuwepo kwa kikundi
hicho kinachojishulisha na kilimo kumeleta faidi kwao hasa kwakuendeshea familia
yao na na kuinua maisha kiuchumi ingawa kuna changamoto ya mashine kukosa mzigo
wa kukoboa kwa wakulima kupungua.
“Walanguzi
wa mpunga kutoka Musoma wamekuwa tatizo la kupungua kwa mzigo wa mpunga wa
kukoboa jambo linalosababishwa na ukosefu wa mtaji wa kununua mpunga wote
unaolimwa kwenye mradi wa Ochuna” alisema Ojijo.
Wakulima
wa mpunga kijijini humo wanalilia vitendea kazi ili waweze kuimarisha kilimo
chao ambacho wanasema kimeanza kuonyesha mafanikio kwa familia zao kwa chakula
na biashara. Faki Mwenda alisema kuwa kuna changamoto ya kiuchumi hasa
kipindi kuanza kilimo kwa wakulima kutokuwa na vitendea kazi.
“Wananchi
hawana vitendea kazi na wanalima kilimo kile cha kizamani ambacho mkulima
alitakiwa kupata gunia 30 kwa hekari anapata gunia 10 na wakati wa kulima
alikopa ng’ombe hivyo nauza mpunga kumfidia mlima hivyo hawezi kujikwamua
kutokana na kilimo cha namna hii… serikali ya awamu ya tano iwawezeshe wananchi
zana za kilimo kupitia vyama vya msingi vya ushirika ili kuinua kilimo chao”
alisema Mwenda.
Vijiji
vya Nyanjage na Ochuna vina zaidi ya hekari 560 zinazofaa kwa kilimo cha mpunga
kijiografia lakini bado serikali haijajikita ipavya kusimamia mradi wa
umwaliaji ambao unaweza kubadilisha wananchi wa wilaya hiyo ambayo kijiografia
ni kame.