WANACHI WAOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI MGOGORO BAINA YAO NA JESHI LA KULINDA WANANCHI JWTZ NYANDOTO.
WANACHI
WAOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI MGOGORO BAINA YAO NA JESHI LA KULINDA WANANCHI
JWTZ NYANDOTO.
Baada ya kuwepo kwa mgogoro wa ardhi baina ya Jeshi
la WananchiJWTZ kikosi cha Nyandoto na wanachi wa Mtaa wa Bugosi kata ya
Nyamisangura Wilayani Tarime Mkoani tangu mwaka 1978 hadi sasa ambapo serikali
imeonekana kufumbia macho suala la
mgogoro huo hali iliyosasabisha wananchi kuiomba serikali ya magufuli
kuingilia kati kwa lengo la kutatua mgogoro huo ili wanachi waendelee na
uzalishaji ikiwepo shughuli nzima ya kilimo ili kuweza kuepuka na balaa la
njaa.
Akizungumza na wananchi wa eneo hilo mkuu wa wilaya
ya Tarime Glorius Luoga baada ya kutembelea maeneo husika ya mtaa huo na
kujionea hali halisi ya mipaka kati ya maeneo ya wananchi na jeshi hilo la
wananchi kikosi cha nyandoto , amewataka
wananchi hao kukaa pamoja na viongoz wao kwa ajili ya kutatua mgogoro huo
ulioonekana kudumu kwa muda murefu bila kutatuliwa huku akiwaahidi wananchi hao
kumaliza mgogoro huo, mara moja, baada ya kukutana na uongozi wa mtaa kwa
kushirikiana na diwani wa kata ya Nyamisangura Bashir Abdallahpamoaj na wanachi
ambao ni wakazi wanaojua historia ya eneo hilo.
Awali mkuu wa wilaya huyo alisema kuwa serikali
inalojukumu la kuchukua eneo lolote kwa ajili ya taasisi yeyote lakini kuna
utaratibu unaofanyika kama wanachi wanamiliki eneo hilo kwa lengo la kuepusha
migogoro ya ardhi na kuwaomab wanchi ho kuwa waturivu kuwa mgogoro huo
utamalizika mapema.
“Mimi nimezunguka hili eneo na kuona kwa macho
nilikuwa nikipata taarifa nikiwa ofisi kuhusu mgogoro huo tutakaa na viongozi
wenu Halamashauri zote mbili ya mji na vijijini ili kuweza kupata suluhu na
kupeleka kwa wakubwa wetu lakini tukiwa tumeisha jilizsha na kushauri ni kipi
kifanyike kwa lengo la kumaliza mgogoro huu lengo ni kumaliza mgogoro”alisema
Dc.
Kwa upande wake diwani wa kata ya nyamisangura ambae
pia ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Tarime Bashir Abdallah
amesema kua wananchi wa eneo hilo wameteseka kwa muda murefu bila ya ufumbuzi
wa suala hilo ,huku akimtaka mkuu wa wilaya ya Tarime kutatua mgogoro huo na
ikiwezekana kulifikisha kwenye uongozi wa ngazi ya juu kwa ajili ya ufumbuzi .
Aidha Diwani
huyo alisema kuwa watu hao walishafanyiwa uthamini tangu zamani lakini serikali
imekaa kimya na wanachi wamesimamishwa shughuli zao za uzalishaji na wanci hao
wako tayari kupisha eneo hilo serikali kama inaliitajia lakini baada ya
kukamilisha utaratibu wote.
“Wanachi wangu wakilipwa fidia eneo wataweza
kuiachia serikali lakini mgogoro huu umechukua muda mrefu na serikali iko kimya
hivyo waziri mwenye dhamana aweze kuingilia kati ili kunusuru hawa watanzania”
alisema Diwani.
Awali nae mwenyekiti wa mtaa wa Bugosi Zacharia
Chacha akimweleza mkuu wa wilaya malalamiko ya wananchi na kumwelekeza mkuu
huyo wa wilaya maeneo yao na wanajeshi wanaosemekana kuwa wamevamia eneo lao
kama wananchina kuweka bikoni suala ambalo limepelekea wanachi hao kusimamisha
shughuli zao.
Kwa upande wao wananchi ambao ni wahanga wa mgogoro
huo wakieleza kero zao mbele ya mkuu wa wilaya ya Tarime wamemuomba mkuu huyo
wa wilaya kutatua mgogoro huo ambao umeonekana kudumu kwa muda wa zaidi ya
miaka thelathini (30) huku wakishukuru ujio wa mkuu huyo wa wilaya huyo kuja
kujinea mwenyewe kwa macho yake .
Inasemekana jumla ya wananchi Miamoja tisini na tisa
199 ambao ni wakazi halali wanaoishi eneo
hilo la mtaa wa bugosi wanategemea eneo hilo kama makazi yao ya kudumu toka
mtoto hadi mjukuu kwa kulitegemea kulima na kujipatia kipato kwa ajili ya kula
na kusomeshea watoto wao .
……………………………MWISHO…………