ANGALIA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI KUHUSU MICHUANO ILIYOANDALIWA KWA LENGO LAKUPINGA UKEKETAJI TARIME.

PICHA YA WASICHANA WACHEZAJI WA TIMU YA SAIRARI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA BANGO LENYE UJUMBE WA KUPINGA UKEKETAJI NA NDOA ZA UTOTONI.

PICHA YA PAMOJA BAINA YA TIMU YA SIRARI VS TARIME MJINI WASICHANA.



Plan International kwa kushirikia na na Umoja wa nchi za ulaya, Jukwaa la utu wa mtoto CDF, na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF wameandaa michezo wa mpira wa miguu kwa watoto wa kike kwa lengo la kupinga Mimba za utotoni , Ndoa za utotoni pamoja na ukeketaji wilayani atoamwameitimisha mashindano ya  mpira wa miguu wilayanI  Tarime Mkoani Mara,
Akiongea na na  jamboleo mratibu wa mradi huo Emmanuel Asaph alisema kuwa lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kupinga ukeketaji na ndoa za utotoni ikiwa ni pamoja na kufikai umjumbe uliokusudiwa kwa jamii kupitia Michezo.

Aidha mratibu huyo alisema kuwa michezo hiyo inahusisha wasichana kwa wavulana pia wameweza kuangalia kata ambazo zinaongoza kwa ukeketaji pamoja na Ndoa za utotoni ili kuweza kufikisha ujumbe sahihi na jamii ibadili mitazamo hasi nakuweza kuondokana na mila potofu zilizopitwa na wakati.
“Michezo inapendwa na watu wengi hivyo kupitia michezo hii tunafikiasha ujumbe sahihi pia kwa ndoa za utotni wanaoani vijana na tumeamua kuweka michezo wa mpira wa miguu kwa wavulana na wasichana ili waweze kushiriki pamoja  ili kubadilishana mawazo” alisema Asaph.

Hata hivyo mratibu huyo aliongeza kuwa wanatarajia kufikia wasichana kuanzia miaka 10-14 wasichana 700 huku miaka 15-18 wasichana600 kwa kipindi cha miaka miwili lengo ni kuhakikisha wanapungauza vitendo vya ukeketaji wilayani Tarime mkoani Mara.

Kariba Jamhuri 14 mkazi wa Nyamisangura ambaye pia ni mchezaji wa mpira wa miguu pamoja na Anna Aizak kidatocha pili katika shule ya sekondari sirari15 walisem akuwa serikali haina budi kuunga mkono mashirika ambayo tayari yamejitokeza kwa lengo la kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ukiwemo ukeketaji na mimba za utotoni.

“Wazazi wetu wamekuwa wakituozesha kwa sababu ya tama ya mali lakini sisi ambao tumejitambua na kupanuka mawazo kupitia michezo hatutakubali kukeketwa pia tutakuwa wabalozi wazuri katika kufikisha elimu stahiki kwa wenetu pia tutaelimisha wazazi ili tuweze kutimiza ndoto zetu”  walisema Mabinti hao.

Kwa upande wake mwalimu wa michezo katika shule ya Sekondari Sirari Bulogo Mbeba alisema kuwa mashindano hayo yawe endelevu kwani yatachangia kwa kiasi kikubwa kufikisha ujumbe kwa jamii kwani michezo inapendwa na watu wengi.

“Mfano ukiangalia uwanjani hapa watu ni wengi hivyo umbe ambao unasambazwa na mashirika hayo utaweza kuwafikia ipasavyo na watu hawa watakuwa wabalozi wazuri kufikasha ujumbe huo kwa jamii huska hivyo michezo ya mpira wa miguu kwa wasichana yasiishie hapa” alisema Mbeba.

Hata hivyo Timu zilikuwa zinaminyana katika uwanja wa Tarasa Sirari kwa upande wa wasichana sirari ilikuwa inaminyana vikali na Timu ya Tarime mjini ambapo Tarime mjini imeilaza Sirari bao 1-0 huku mpira wa miguu kwa wanaume ilikuwa ni Sirari ikiminyana vikali na Ng’ereng’ere ambapo Sirari iliibuka kidedea kwa kuilaza Ng’ereng’ere bao 2-1.

........Mwisho...


Powered by Blogger.