GRACA MACHEL TRUST FUND KUFIKIA WATOTO WASHULE 20,000 MKOANI MARA.

PICHA YA GRACA MACHEL KATIKATI BAADA YA KUTIA SAINI HII LEO KWENYE UZINDUZI WA MFUKO WA GRACA MACHEL TRUST FUND KWA AJILI YA KUSAIDIA WATOTO WA SHULE ZA MSINGI 20,000 KATIKA WILAYA ZOTE ZA MKOA WA MARA KWA KIPINDI CHA MIAKA MIWILI KUTOKA KWA GRACA MACHEL KUSHOTO NI MKUU WA MKOA WA MARA MAGESA MULONGO KULIA NI ASKOFU WA KANISA CATHORIC JIMBO LA MUSOMA MAICHAEL MSONGANZILA.



GRACA MACHEL TRUST FUND KUFIKIA WATOTO WASHULE 20,000 MKOANI MARA.

Aliyekuwa mke wa Rais  mstaafu wa wa Afika kusini Nelson Mandela amezindua mfuko  ambao unatarajia kufikia watoto 20,000 ambao wamaeacha shule katika mkoa wa Mara kutokana na shughuli mbali mbali mbali za Uchumbaji wa Madini, Uvuvi na Bihashara pamoja na changamoto zinzokabili familaA zikiwemo na mila na desturi potofu zinazoendekezwa na baadhi ya makabila yote yaliyomo ndani ya mkoa wa Mara.

Akizindua mradi huo katika ukumbi wa mwekezaji musoma  Musoma Graca Machel alisema kuwa lengo la mradi huo ni kufikia watoto 20,000 kutoka katika shule za msingi ambao wameacha shule huku wakilenga hasa watoto wa kike ili kuhakikisha wanatimiza ndoto zao katika sula zima la Elimu.

Aidha Graca Machel aliongeza kuwa kutokana na mradi huo watasaidiana na viongozi wa srikali kutoka ngazi zote ikiwemo jamii katika wilaya zote za mkoa wa Mara kwa kipindi cha miaka Miwili ambapo mwaka mmoja wanajarajia kufikia watoto Elfu kumi na mwaka wa pili Watoto Elfu kumi
Kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini pamoja na uvuvi na bihashara ndogondogo kwa watoto wadogo kuanzia mwaka 2008 mpaka 2014 watoto Elfu kumi na Moja  hawakubahatika kumaliza masomo yao katika shule za msingi hivyo kutatua changamoto hiyo inayokabili mkoa wa Mara wameamua kuanzisha mfuko huo kwa lemmgo la kuwakiomboa watanzania. 

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Mara Magesa Mulongo alisema  kuwa kulingana na Tafiti zilizofanywa na mashirika likiwemo shirika la Unicef limebaini kuwa watoto Elfu Hamsni na Tisa ambao wanatarajia kuwa shuleni  shuleni shule za msingi na Sekondari hawapo shuleni.  

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa maofisa Elimu, Watendaji wa serikali pamoja na walimu kuhakikisha watoto wote wanakuwa shuleni ili badae waweze kutumikia Taifa.

Tutaanza zoezi hili mara moja sisi kama mkoa tumepokea vizuri sana juhudi za huu mfuko wa Mama yetu Graca Machel na ninasema kuwa nitahakikisha nasimamia sana huu mradi kwa lengo la kutimiza lengo alisema Mulongo.

Michael Msonganzila ni Askofu mkuu wa kanisa kathoric jimbo la Musoma alisema kuwa  kuwa ushirikano na mshikamano wa makundi mbalimbali ya watu yatafanikisha kwa mradi huo ambao umetolewa na wahisani hao.
Askofu alisema kuwa viongozi wa dini wataendelea kuelimisha jamii ili kuwza kuondokana na mila na desturi ambazo zimekuwa zikimukandamiza mtoto wa kike nakupelekea kuacha masomo katika shule za msingi na sekondari.

Ostack Mligo ni katibu wa Mara Alliance alisema kuwa suala hilo limefanikiwa baada ya kuunda muungano wa mashirika ya kidini, Serikali na Yasiyokuwa ya kiserikali 13 kwa lengo la kuwakomboa watoto Elfu ishiri  ambao wameacha shule.

 Musa Bomani kwa niaba yaw zee wa mila mkoani mara alisema kuwa wzee wa mila watahikikisha wanaendelea kupinga mila na desturi ambzo zinasababisha watoto kuacha shule kwa ni elimu yao ni haki yao ya kimusingi.
Muradi huo utaanza katika wilaya ya Bunda, Tarime, Musoma Rorya na Butiama ambapo wanatarajia kufikia watoto Elfu Ishirini kwa kipindi cha miaka miwili huku mwaka mmoja wakianza na watoto Elfu kumi tu
………..Mwisho…..
Powered by Blogger.