SHULE MBILI ZA MSINGI ZA TUMIA MADARASA MATANO HUKU BAADHI WAKISOMEA CHINI YA MITI.
Na Frankius
cleophace Tarime.
SHULE MBILI ZA MSINGI ZA TUMIA
MADARASA MATANO HUKU BAADHI WAKISOMEA CHINI YA MITI.
Ukosefu wa
huduma ya miundombimu ya barabara Afya na Maji katika kata ya Kwihacha Wilayani
Tarime Mkoani Mara inapelekea kukwamisha maendeleo ya jamii ambayo inapelekea
wanafunzi kutembea umbali mrefu kwa lengo la kufuata huduma ya Elimu, akina
mama huduma ya Afya ambpo imepelekea pia shulu mbiliz a msingi kutumia vyumba
vitano vya madarasa na baadhi ya wanafunzi kusomea chini ya Miti katika shule
ya msingi Gibaso na Kwihancha.
Aidha katika
shule ya Msingi Gibaso na Kwihacha
kutoka na upungufu wa vyumba vya madara kumepelekea shule mbili kuchangai
vyumba vitano vya madarasa suala ambalo limepelekea wanafunzio kusomeachini ya
Miti jambo ambalo linaweza kupeleakea
kushuka kwa taaluma wanafunzi katika shule hizo mbili
Marwa Marco ni mtendaji wa wa kata ya Kwihancha akibainisha chngamoto
hizo mbele ya Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini kupitia cham cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA John Heche katika mkutano wa Hadhara alisema kuwa upungufu
huo wa madarasa umepelekea shule hizo mbili kuchangia madara ili wanafunzoi hao
waweze kupata haki yao ya msingi ya kielimu.
Hata hivyo
Mtendaji huyo alibainisha kuwa vijiji vitatu vinachangamoto ya upatikanaji wa
maji safi na salama pamoja na vituo vya zahanati katika kjiji cha Nyabirongo na
Karagatonga ambapo inapelekea akina mama kutembea umbali mrefu kwa lengo la
kufua Huduma ya Afya.
John Heche
ni mbunge wa jimbo la Tarime vijijini kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo
CHADEMA katika mkutano huo wa hadhara alisema kuwa kwa ujumla hali ya elimu
katika jimbo lake ni mbaya hivyo wanapaswa kutumia nguvu kubwa kwa lengo la
kutatua elimu.
Aidha Mbunge
huyo alisema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kupitia vyanzo vyake vya
ndani wametenga Millioni 350 kwa ajili ya ununuzi wa madawati ili kuondoa hadha
ya kuka chini.
Aidha mbunge
huyo alisema kuwa kwa miaka miwili atahakikisha kila mwanafunzi anakali dawati
ili kuondoa changamoto ya kukaa chini
“Namimi kama
mbunge wenu sijalala nitahkikisha nafanya kazi kwa kutumia fedha zangu na za
mfuko wa jimbo ili kuweza kuboresha sekta ya Elimu na Afya” alisema Mbunge.
Kwa upande
wake Diwani wa kata ya Kwihancha Mustapha Masian aliesema Tembo wamekuwa kero
kwa kuaharibu mazao ya wanachi bila kulipwa fidia ambapo amemwomba mbunge kusaidia
suala hilo.
Aidha Diwani
huyo alisema kuwa katika kipindi chake kilichomalizika akiwa diwani ameweza
kupigia kelele suala la kulipwa fidia lakini hajasikilizwa na sasa amepewa
dhamana ya kuongoza tena ivyo amemwomba mbunge kuchukulia uzito mkubwa ili
kuweza kuwakomboa wanachi hao.
‘Kata yangu
ya Kwihancha kunachangamoto ya ukame wanachiu wanajitahidi kulima lakini bado
mazao yao yanaharibiwa na Tembo na serikali haifanyi juhudi zozote kwa lengo la
kuwalipa fidia wanchi wangu hili jambo limeniumiza kichwa” alisema Diwani huyo
……Mwisho….