Serikali yaombwa kutoa mafunzo kwa walimu wa Michezo.
Serikali yaombwa kutoa mafunzo kwa
walimu wa Michezo.
Serikali
kupitia waziri wa Habari, Utamaduni sanaa na Michezo Nnape Nnauye imeombwa
kutoa mafunzo maalumu ya Michezo kwa walimu wa michezo katika sekondari hapa
Nchini ikiwa ni pamoja nakuboresha
Mitahala katika Vyuo , vikuu kwa lengo la kuboresha sekta ya Michezo.
Hayo
yamebainishwa na Mwalimu wa Michezo katika shule ya sekondari Sirari wilayani
Tarime mkoani Mara Mwl Bulogo Mbeba
katika kuitimisha michezo ambayo imeandaliwa na shule hiyo kwa lengo la
kuibua vipaji mbalimbali.
Aidha
Mwalimu huyo wa michezo alisema kuwa shule za sekondari zimekuwa zikikumbwa na
changamoto ya walimu wa michezo ambao wamwsomea sekta ya michezo pia walimu
waliopo wamekuwa wakitumia uzoefu kwa ajili ya kuendesha michezo hivyo
wameiomba serikali kuwapa mafunzo walimu hao kwani kanuni za michezo zimekuwa
zikibadilika kila kukicha.
Hata hivyo
Mbeba aliongeza kuwa una umuhimu wa kuboresha mitahala katika vyuo vikuu kwa
lengo la kuborsha michezo ikiwa ni pamoja na kutengwa kwa fedha za kutosha ili
kusimamia ipasavyo michezo katika shule za sekondari.
Mwalimu huyo
alisema kuwa shule hiyo ya sekondari imnakumbwa na changanmoto ya ubora wa
viwanja pamoja na vifaa vya michezo hivyo alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau na
wapennzi wa michezo kujitokeza kwa lengo la kutatua changamoto hiyo ili
kuboresha michezo shuleni hapo.
Joel Mwita
amabaye ni mwenyekiti wa bodi ya shule sirari amedhamini michezo hiyo kwa lengo
la kuboeresha sekta ya michezo katika shule za sekondari.
Joel alisema
kuwa ametambua umihimu wa michezo katika sekondari na kuamua kudhamini michezo
hiyo huku akidai kuwa michezo ni furaha na michezo ni Afya kwani itasaiadia
kupunguza utoro kwa wanafunzi.
“Pia shule
hii imeanzishwa na sisi wazazi na walezi kwahiyo ni wajibu wetu kudhmini
michezo ili watoto wetu waweze kucheza na kufurahi sana” alisema Joel.
Michezo hiyo
imeambatana na zawadi mbalimbali ambapokwa upande wa mpira wa miguu mshindi wa kwanza ambaye ni kaidato cha Pili
baada ya kulaza kidato cha tatu kwa bao1-0 kupitia kwa mchezaji Taban John
dakika ya 50 kipindi cha pili na kuweza kujinyakulia zawadi ya Mbuzi mmoja.
Upande wa mpira wa Pete mshindi wa kwanzakidato
cha Nne na kuweza kujinyakulia mbuzi mmoja huku wachezaji mbalimbali na
washindi wa michezo ya Wavu, kukimbia wameweza kujinyakulia zawadi mbalimbali
zikiwemo fedha taslimu kuanzia Elfu ishirii, Thelathini na Hamsini kwa lengo la
kutoa hamasa ya katika Michezo.
Naye Mwalimu
mkuu wa shule hiyo Jonathan Masambu amewataka wanafunzi hao kupenda michezo
kwani michezo ni ajira.