HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME YAKATAA SHILINGI 1’060,127,035.44 KUTOKA ACACIA.

PICHA YA HUNDI ILIYIKATALIWA NA HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME MKOANI MARA.


HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME YAKATAA SHILINGI 1’060,127,035.44 KUTOKA ACACIA.

Halmashauri ya wilaya ya Tarime imekataa kupokea hundi ya shilingi Billioni moja na millini sitini kwa ajili ya ushuru wa huduma  ambazo ulipwa na mgodi wa uchimbaji wa dhahabu ACACIA uliopo Nyamongo wilayani Tarime Mkoani Mara kwa kile ambacho Halmashauri imetaka kujua fedha hizo zinazotolewa zinaendana za uzalishaji wa Mgodi huo kwa kipindi cha miezi sita.

Akifungu kikao kabla ya kupokelewa kwa hundi hiyo yenye thamiani ya shingi 1’060,127,035.44 Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime Moses Yomami amesema kuwa Halmashauri yake haitakuwa tayari kupokea hundi hiyo kabla haijajilizisha kuwa mgodi unachozalisha na kile wanachotoa vinaendana huku akiutaka mgodi huo kukabidhi hundi katika baraza la madiwani ambalo linatarajia kufanyiaka Feburuari 10 mwaka huu wakiwemo wananchi ili waweze kujilizisha.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa hapo nyuma Halmashauri hiyo ili kuwa ikipoteza mapato makubwa yanayotokana na uzalishaji wa Mgodi huo kwa sababau ya kukiuka baadhi ya sheria jambo ambalo hatoweza kulifumbia macho kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.

Alisema kuwa Halmashauri yake ilitaka kujua  katika miezi sita mgodi huo umeweza kushalisha kiasi gani kulingana na fedha hizo ambazo wameiletea Halmashauri hiyo.

“Mimi kama Mwenyekiti wa Halmashauri hii nitaendelea kusimamaia sheria kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo kwa sababu mgodi huuu kabla ya sisi Halmashauri hii ilikuwa ikipoteza mapata huku wakiweka Akaunti fedha na badae kutukabidhi hundi pasipokupiga mahesabu jambo ambalo nimelikataa leo” alisema Mwenyekiti.


Athumani Akalama ni mkurugenzi wa Halmashauri yawilaya ya Tarime akiongea na waandishi wa abari alisema kuwa kilichokuwa kinachohojiwa na wajumbe wakiwemo madiwani na watumishi wa Halmashauri nikutaka kujua kuwa kikosahihi kulingana na uzalishaji wao nakusema kuwa kuwa tukio hilo lilikuwa kubwa ilibidi washirikishwe madiwani wote  katika kikao.

“kwa sababu tunakikio cha baraza la madiwani tarehe kumi kama mwenyekiti alivyosema basi zoezi hilo limeweza kusitishwa na kufanyika tarehe kumi katika baraza la madiwani hao” alisema Mkurugenzi.

Kwa upande wake Meneja wa Mgodi wa ACACIA Garry Cheap Man ni jambo la kushangazaa kukataa kupokelewa kwa fedha hizo huku akisema kuna  kuwa kama kuna mashaka wako huru kwenda kufanya ukaguzi ili kujilidhisha.

Hata hivyo mwenyekiti huyu ameuagiza mgodi huo kubainisha makampuni yote yanayofanyakazi katika mgodi huo kwa lengo la kulipia ushuru ili halmashauri hiyo iweze kuongeza mapato kwa lengo la kufanya kzai za maendeleo ya wananchi ikiwemo ujenzi wa zahanati kwa kila kijiji.

Fedha hizo zitakabidhiwa Februari kumi mwaka huu mbele ya kikao cha madiwani  baada ya mgodi huo kubainisha kile ambacho Halmashauri inahitaji
                            …….Mwisho……


Powered by Blogger.