Serikali yaombwa kutatua changamoto katika shule za misingi Tarime.
PICHA YA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI NYANDOTO DARASA LA TATU WAKIWA WAMEKAA CHINI SAKAFUNI WAKATI WAKIENDELEA NA MASOMO.
Serikali yaombwa kutatua changamoto
katika shule za misingi Tarime.
Serikali
imeombwa kutatua chanangamoto ya upungufu wa madawati katika shule za msingi
Katika Halmashauri ya mji wa Tarime ili
wanafunzi waondokane na hadha ya kukaa chini wakati kujifunza kwa lengo la
kuboresha taaruma, kwani baada ya serikali kutangaza elimu bure baadhi ya shule
zinakumbwa na changamoto ya uhaba wa madarasa pamoja na madawati suala ambalo
linapelekea asilimia kubwa wanafunzi wa awali na chekechea kusomea chini .
Hayo
yamebainishwa katika shule ya msingi
Nyandoto kipindi wakipokea msaada wa mifuko 30 YA saruji kutoka kwa aliyekuwa mgombea ubunge
jimbo la Tarime mjini kupitiaCCM Michael Kembaki na Bank ya NMB Tawimla Tarime kwa lengo la kuunga nguvu za wananchi katika
ujenzi wa vyumba viwilli vinavyojengwa na ofisi ya walimu shuleni hapo.
Katika
kutatua baadhi ya changamoto zinazozikumbz shule za msingi katika Halmasauri ya
mji wa Tarime aliyekuwa mgombea ubunge
jimbo la Tarime Mjini Michael Kembaki ambaye pia ni mkurugenzi wa Memolial
Foundatin iliyopo jijini Arusha ametoa mifuko 20 ya saruji katika shule ya
msingi Nyandoto pamoja na mifuko 20 katika shule ya msingi Nyansurura huku
banki ya NMB ikitoa mifuko 10 ambapo shule ya msingi Nyandoto imepata jumala ya
Mifuko 30 ya saruji.
Aidha
Michael Kembaki alisesema kuwa ameamua kutoa msaada huo kwa lengo la kuunga
juhudi za serikali ya hawamu ya Tano kwani baadhi ya misaada hiyo ni ahadi
alizozitoa katika kipindi cha kampeni hivyo anatekeleza kwa lengo la kupunguza
baadhi ya changamoto zinzowakabili wanafunzi baada ya serikali kutangaza elimu
bure wanafunzi wa awali na chekechea wameandikishwa kwa wingi nakupelekea
upungufu wa madarasa huku wakisomea chini ya miti.
“Ni moja ya
kutimiza ahadi zangu ambazo niliweweza kuhaidi kipindi changu cha kampeni kuwa
kila sule ya msingi ambayo inaboma lazima niweze kutoa usirikiano kwa lengo la
kuunga juhudi za wanachi” alisema Kembaki.
Naye Diwani
wa kata ya Nyandoto Fredirick Sabega alisema kuwa kwa lengo la kunusuru shule
za Msingi ambazo zimo ndani ya kata ya Nyandoto atahakikisha anatafuta nakuomba
wadau mbalimbali wakiwemo wafanunyabihashara
kwa lengo la kutatua changamoto za shule za msingi.
“Nimekuwa
nikitafuta wadau mbalimbaliwakiwemo wadau wa banki ya NMB leo katika shule ya
Nyandoto wamweza kutoa msaada wa mifuko Kumi pia aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Tarime Mjini (CCM)
Michael Kembaki ametoa mifuko 40 ya saruji
katika shule ya Msingi Masurura na Nyansurura na juzi alitoa mifuko 20
katika shule ya Msingi Nyagasese hivyo juhudi zake zinzonesha ni kiasi gani
anajali wananchi wa Tarime” alisema Sabega.
Kwa upande
wake Mwalimu mkuu wa shule ya Msnigi Nyandoto Zacharia Bunyaga alitoa sukrani kwa kupata mifuko 30 ya saruji
huku akibainisha changamoto zinazoikabili shule kuwa ni pamoja na upungufu wa
madarasa ambapp hitaji 08 yaliyopo 06 huku vyumba viwili vikiwa chakavu numba
za walimu hitaji 08 zilizopo 02 ofisi za walimu hitaji zilizopo 02 huku shule hiyo ikiwa na jumla ya wanafunzi
296,
Aidha
Mwalimu alisema kuwa kuligana na juhudi za serikali kuwa elimu bure wazazi na
walezi wameweza kuwa na mwamko mkubwa wa elimu shule hiyo waligemea kuandika wanafunzi 42 darasa la
kwanza lakini mpaka sasa wameandikisha wanafunzi 58 na awali walitarajia 30
lakini wameweza kuandikisha wanafunzi 58.
Hata hivyo
shule ya Msingi Nyandoto wanafunzi wa darasa la tatu wanakumbwa na changamoto
ya kusomea chini kwenye vumbi kwa sababu ya kukosa madawati huku darasa la siti
wakisomea kwenye jingo ambalo halijamalizika huku wakisubiri wanafunzi wamalize
masomo ili kuwapisha kwa lengo la kuendelea na masomo.
“Sisi darasa
la sita darasa tunalosomea hakuna madirisha wala mabati mvua ikinyesha
inatunyeshea pamoja na jua tunaomba changamoto hii serikali iweze kutatua”
walisema wanafunzi hao.