Chekechea, la Kwanza darasa la pili na la Tatu wasomea darasa moja Sule ya Msingi Nyagasese.
Chekechea, la Kwanza darasa la pili
na la Tatu wasomea darasa moja Sule ya Msingi Nyagasese.
Kulingana na
sera ya Serikali ya hawamu ya Tano kuhusu Elimu bure kuanzia shule za msingi na
Sekondari serikali imeombwa kutatua changangamoto inayoikabili shule ya msingi
Nyagasese iliyopo kata ya Nyandoto Halmashauri ya mji wa Tarime.
Akiongea na
blog hili mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Nyagasese Mwl Sevelin Isaka alisema
kuwa shule hiyo inakumbwa na chanagamoto nyingi ikiwemo muruyndikano wa wanafunzi madarasani ambapo
darasa moja ukaa wanafunzi zaidi ya 65.
Mwalimu mkuu
alisema kuwa kulingana na upungufu wa madara wanafunzi wa darasa la Awali na la
kwanza wanasoma chumba kimoja na darasa la pili na la tatu wanasoma chumba kimoja suala ambalo
linawakanganya katika ufundishaji na jambo hilo linaweza kupelekea kutofaulu
kwa wanafunzi hao.
Changamoto
nyingine ni upungufu wa walimu kwani shule hiyo inawalimu wawili kati ya
watano,upungufu wa vitabu pamoja na fedha za ruzuku kwa ajili ya kuendesha
shule hiyo ambayo kwa sasa inaishia darasa la tatu.
“Shule yangu
ni change lakini bado inakumbwa na changamoto kubwa lakini ujenzi wa madarasa
unaojengwa kwa nguvu za wananchi serikali haina budi kuweka mkono wake kwa
lengo la kuboresha elimu” alisema Mwalimu.
Katika
kuunga juhudi za elimu bure na kuboresha miundombinu ya shule hiyo aliyekuwa
mgombea wa ubunge jimbo la Tarime Mjini Michael Kembaki kupitia chama cha Mapinduzi
(CCM) ametoa mifuko 11 ya saruji pamoja na nondo11 kwa lengo la kuendeleza
ujenzi wa madarasa mawili yanayoendelea shuleni hapo kutokana na nguvu za
wananchi.
Kembaki alisema
kuwa akiwa katika kampeni zake aliweza kutoa ahadi kuwa awe kiongozi au hasiwe atahakikisha
anaunga juhudi za wananci katika kuborsha elimu katika shule za msingi pamoja
na suala zima la maendeleo.
“Mimi katika
kampeni zangu niliweza kutoa ahadi nyingi na pia niatendelea kuzitekeleza kwa
lengo la kujenga Tarime bila kujali itikadi za vyama au kuwa sikubahatika
kupata ubunge lakini kiu yangu kubwa ni kusaidiia wananchi wangu” alisema
Kembaki.
Hata hivyo
kembaki alisema kuwa hivi karibuni atapelea mifuko 20 ya suruji katika shule ya
msingi Masurura na shule ya msingi Nyandoto Mifuko 20 lengo ni kuunga serikali
kuhusu Elimu bure kwani wanafunzi wameandikishwa wengi na shule nyingi
zinakumbwa na upungufu wa madaras.
Fredirick
Sabega ni diwani wa kata ya Nyandoto kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akipokea
msaada huo alisema kuwa ataendelea kutafuta wadau mbalimbali kwa lengo la
kupunguza baadhi ya changamoto zinazoikumba shule hiyo.
Hata hivyo
aliongeza kuwa kulinganana kasi ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John
Magufuli wananchi hawana budi kuendelea kushirikiana kwa pamoja kwa lengo
lakuleta maendeleo na siyo kutegemea kila kitu kutoka srikalini.
Shule ya
Msingi Nyagasese inajumla ya wanafunzi 233 jumla ya walimu watatu na jumla ya
madarasa mawili uku itaji ikiwa ni madarasa Manne hivyo wameiomba serikali kwa
kushirikiana na Halmashauri ya Mji wa Tarime kusikiliza kilio hicho na kuweza
kutatu ili kuweza kuwaandalia mazingira mazuri ya Elimu kwa watoto hao.