WAZIRI ATOA AGIZO KWA WAZAZI NA WALEZI KUPELEKA WATOTO SHULE.
Picha ya waziri
wa Nchi ofisi ya waziri mkuu, sera
uratibu na watu wenye ulemavu Jenista
Mhagama alipokuwa anafanya mahojiano na waandishi wa habari katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Simiyu Eraston Mbwilo.
WAZIRI ATOA AGIZO KWA WAZAZI NA
WALEZI KUPELEKA WATOTO SHULE.
Baada ya
kufutwa kwa ada katika shule za msingi na sekondari Serikali imesema kuwa kila
mzazi au mlezi ahikikishe watoto wote wanapelekwa shule ikiwa ni pamoja na kila
shule ya msingi kuwa na madarasa ya chekechea na awali kwa ajili ya maandalizi
ya watoto hao ili kuweza kuunga sera za serikali katika kuhakikisha kila
Mtazania anapata Elimu.
Kauli hiyo
imetolewa hivi karibuni na waziri wa
Nchi ofisi ya waziri mkuu, sera uratibu
na watu wenye ulemavu Jenista Mhagama
alipokuwa kuwa katika ziara yake Mkoani Simiyu katika kikao cha majumuisho
kilichofanyika kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa simiyu Eraston Mbwilo.
Aidha Waziri
huyo amesema kuwa baada ya serikali kufuta ada katika shule za msingi na
sekondari ni jukumu la kila mzazi au mlezi kuhakikisha watoto wote wanapelekwa
shule huku wakinunuliwa sare za shule.
Hata hivyo mhagama
amesema kuwa kila Halmashauri hapa nchini zihakikishe zinztenga maeneo maalumu
kwa ajili ya uzalishaji kwa vijana ili vijana hao waweze kujiongezea kipato
kutikana na uzalishaji huo huku wakianzisha viwanda vidogovidogo na serikali
itaweza kusaidia kukuza viwanda hivyo.
Hata hivyo
jenista ameziagiza Wilaya hapa Nchini kuhakikisha zinafanya ukaguzi ili
kuhakikisha wageni wanaofanya kazi katika viwanda kuwa na vibali rasmi huku
wakihakikisha watumishi wa serikali na binafsi pamoja na vijana wanapatiwa mikataba mahali pakazi.
Eraston
Mbwilo ni Mkuu wa mkoa wa simiyu amesema kuwa kulingana na maagizo ya waziri
uyo atahakikisha wanayafanyia kazi kwa lengo la kuleta maendeleo ndani ya mkoa
huo huku akiahaidi kukutana na wakurugenzi wote maofisa elimu msingi na
sekondari pamoja na waratibu Elimu kwa lengo la kuweka mikakati juu ya agizo la
Waziri.