Mbunge Rorya nitahakikisha nasimamia fedha za Halmashauri.


Mbunge Rorya nitahakikisha nasimamia fedha za Halmashauri.

Mbunge aliyechaguliwa Jimbo la Rorya kupitia chama cha mapinduzi CCM ambaye pia alikuwa akitetea kiti chake Lameck Airo ambaye ameibuka mshindi kwa kupata kura a 59,919 huku mpinzani wake  kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA  Steven Howawa ambaye alipata kura 42,532 amewambia wananchi kuwa atahakikisha anasimamia fedha za kutekeleza miradi ya Wananchi   katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya ikiwa ni pamoja na kujenga Nyumba za walimu katika shule za Msingi na Sekondari huku akitatua Changamoto ya Maji.

Haya yamebainishwa kipindi Mbunge huyo alipokuwa akiongea na wananchi wa Wilayani Rorya Mkoani Mara katika Sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya Utegi kwa ajili ya kuwashukuru wananchi hao kwa kumuchagua kwa awamu ya pili.

Lameck alisema kuwa ili kuweza kuwakomboa wakazi wa Rorya atahaikisha anasimamia vyema fedha za miradi ya wanachi zinazoletwa katika Halmashauri kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili wananchi hao.
"Mmenichagua kwa awamu ya pili kwa sababu munaimani kubwa na na Mimi nawambia tena nitahakikisha natimiza ahadi zote tulizohaidi katika mchakato mzima wa kampeni zetu" alisema Lameck.

Hata hivyo mbunge huyo alisema kuwa  kuwa katika Wilaya ya Rorya ili kuondokana na janga la Njaa ambalo limekuwa likiwakabili mara kwa mara atahakikisha kunaanzishwa kilimo cha bihashara kama vile Alizeti na karanga ili kuweza kuwakomboa wananchi hao,

"Mazao ya chakula wananchi wamekuwa wakilima na badaewafanyabihashara kutoka nchi jirani ya Kenya wanapoingia Wilayani humu wananunua zao hilo la chakula na kwa sababu wananchi wanakuwa wanataka kulipa karo za watoto hulazimika kuuza chakula chote lakini tumeisha weka mikakati ya kuanzisha zao la bihashara ili waondokane na kuuza chakula na badae kukumbwa na Njaa" alisema Mbunge.

Katika Sherehe hizo Mkuu wa Wilaya ya Rorya Felix Lyaniva amewapongeza wananchi hao kwa kufanya uchaguzi wa Amani huku wakikitendea haki chama cha Mapinduzi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilayani RoryaSamwel Kiboye akitoa shukrani kwa ajili ya Chama amesema kuwa wananchi wamefanya maamuzi mazuri kuchagua chama cha mapinduzi nakudai kuwa chama kitaenda kuwashughulikia viongozi walikuwa wanashika chama miguu wakati wa kampeni kwa  lengo la kujenga chama.

"Kuna baadhi ya viongozi wa chama chetu wametushika miguu katika kipindi chetu cha kampeni sasa tunaenda kuwashughulikia kwa lengo la kujenga Chama" alisema Kiboye.
Mwenyekiti alidai kuwa baadhi ya viongozi wa chama hicho walikuwa wanampinga mgombea ubunge pamoja na madiwani wake jambo ambalo chama hicho alitafumbia macho kwa lengo la kulinda heshima ya chama na kurudisha maadili kwa wananchama wake.
........Mwisho.....
Powered by Blogger.