AKUTWA AKIWA AMEUWAWA,MFANYABIASHARA AVAMIWA NA KUPORWA FEDHA.

AKUTWA AKIWA AMEUWAWA,MFANYABIASHARA AVAMIWA NA KUPORWA FEDHA.

MTU mmoja ambaye hajafahamika jina lake amekutwa akiwa ameuwawa katika barabara itokayo katika Kitongoji cha Forodhani kwenda kijiji cha Sokoni Kata ya Sirari Wilayani Tarime mkoani Mara.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya Lazaro Mambosasa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo,alisema kuwa mnamo Octoba 27,2015  Askari wakiwa doria walimkuta mtu mmoja mwanaume (25-30) ambaye jina na anuani haijafahamika akiwa ameuwawa.

Mambosasa alisema kuwa alikutwa ameuwawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kifuani mara mbili upande wa kushoto na mtu/watu wasiyofahamika.


Alisema kuwa chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya halmashauri ya mji Tarime kusubiri uchunguzi wa Dactari.

Wakati huohuo, Majira ya saa saba usiku Octoba 27,2015 katika kitongoji cha Nyairoma,Kijiji cha Sokoni kata ya Sirari Wilayani hapa,John Chacha (46) Mfanyabiashara wa samaki na mkazi wa kitongoji cha Nyairoma akiwa amelala nyumbani kwake alivamiwa na majambazi.

Mambosasa alisema kuwa alivamiwa na majambazi wapatao 8 ambao hakuwatambua wakiwa na bunduki aina ya SMG/SAR.Mapanga na mashoka na kumnyang’anya fedha milioni  4,000,000 .

“Wakati wa wizi huo walifyatua risasi tano hewani na kumshambulia kwa kumpiga bapa la panga kwenye mkono wa kushoto na hali yake inaendelea vizuri na baada ya tukio hilo majambazi walikimbia kuelekea nchi jirani ya Kenya”alisema Mambosasa.

Alisema kuwa hakuna mtu/watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo nakwamba mbinu iliyotumika ni kuvunja mlango kwa kutumia shoka na kufyatua risasi hewani na yaliokotwa maganda mawili aina ya SMG/SAR eneo la tukio na juhudi za kuwatafuta waliotenda uhalifu huo zinaendelea.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,MWISHO,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Powered by Blogger.