GARI LA SERIKALI LAUWA 4 RORYA

GARI LA SERIKALI LAUWA 4 RORYA
WATU wanne wakazi wa Wilayani  Rorya mkoani Mara  wamegongwa  na Gari la Serikaliwakiwa wanatembea kwa miguu   lenye namba za usajili STK 7142  Toyota Land Cruiser ilikokuwa ikiendeshwa na Lameck Gerlad Sembuche (44).

Kamanda wa Polisi mkoa Tarime/Rorya Lazaro Mambosasa alisema majira  ya saa  3 usiku  Octoba 26,2015. Katika kijiji cha Makongoro,kata ya Rabouro,Wilayani Rorya  Mtuhumiwa alimgonga Osewe Olando(45),Bilishan Kagose(19),Rose Wambogo(9)na Debora Samsoni wote wakazi wa kijiji cha Kassino.

Mambosasa alisema aliwagonga na kuwasababishia vifo vyao papohapo na chanzo cha ajali ni kuzima  kwa taa za gari ghfla wakati likiwa kwenye mwendo nakwamba mtuhumiwa amekamatwa na gari lipo kituo cha polisi Tarime.

Wakati huohuo  mnamo  Octoba 26, majira ya  saa sita mchana katika kijiji cha sokoni,Kata ya Sirari,Wilayani Tarime Gari lenye namba za usajili T.562 CAP aina ya YUTONG iliyokuwa ikiendeshwa na Joseph Magazin ikitokea katika kituo cha mabasi cha Sirari kuelekea katika egesho la kituo cha  mafuta ilipigwa mawe .

Mambosasa alisema gari hilo lilishambuliwa kwa kurushiwa mawe na kuvunjwa kioo cha mbele,vioo vinne vya madirisha upande wa kulia na vioo vitatu vya madirisha upande wa kushoto vyote vikiwa na thamani ya 6,500,000.

Aliongeza kuwa siku hiyohiyo gari  linguine lenye namba za usajili T.925 CZM aina ya YUTONG iliyokuwa ikiendeshwa na Ezekia  Merico(32) Dereva mkazi wa Isamilo Mwanza ilishambuliwa kwa mawe na kuvunjwa kioo kimoja cha Dirisha la nyuma upande wa kulia lenye thamani ya 2,000,000.

Mambosasa alisema kuwa  Magari hayo ni mali ya Kampuni ya Zakaria Express,nakwamba watuhumiwa wawili wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo ambao ni Libaya Msabi (34)mkazi wa Remagwe na Marwa Juma(17) mkazi wa Sokoni Sirari nakwamba chanzo cha tukio ni ushabiki wa kisiasa.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,MWISHO,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Powered by Blogger.