ESTHER MATIKO AIBUKAMSHINDI TARIME MJINI KWA KURA 20017

Na Frankius Cleophace Tarime.
ESTHER MATIKO AIBUKAMSHINDI TARIME MJINI KWA KURA 20017

Aliyekuwambunge wa viti maalumu kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Esther Matiko na Mgombea Ubunge jimbo la Tarime Mjini ameibuka kidedea kwa kura 20017 huku akifuatiwa na Mgombea Ubunge jimbo la kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Michael Kembaki kwa kura14,025 akifuatia mgombea wa ACT Wazalendo Deogratias Meck kwa Kura 356.

Akitangaza matokeo hayo Msimamizi mkuu wa Uchaguzi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Juma Mwajombe amemutangaza Esther Matiko kuwa mshindi katika Jimbo hilo kupitia Chama cha Upinzani huku akifuatiwa mgombe Ubunge kupitia CCM na wa Mwisho ACT Wazalendo.

Akiongea na wandishi wa habari Mgombea ubunge jimbo la Tarime Mjini kupitia upinzani Esther Matiko amesema kuwa wanatarime wategemee maendeleo ya haraka ikiwa ni pamoja na kudai kuwa watanzania wameweza kudhiilishia umma kuwa Mwanamke anaweza kuongoza vyema.

Hata hivyo Matiko ameongeza kuwa kulingana na kura ambazo wamemuchagua wananchi wa Tarime hatoweza kuwaangusha katika suala zima la Maendeleo ikiwa ni pamoja na kutekeleza ahadi zote ambazo aliweza kuhaidi katika kipindichote cha kampeni.

Mpaka sasa tunatarajia kupata matokeo ya Ngazi ya Udiwani kata zote Nane zinazotengeneza jimbo la Tarime Vijijini pamoja an Matokeo ya Jimbo la Tarime Vijijini.
                                ...Mwisho....
Powered by Blogger.