MATIKO NITABORESHA VYANZO MAPATO



MATIKO NITABORESHA VYANZO MAPATO


MGOMBEA Ubunge jimbo la Tarime Mjini wa Chama cha Demkorasia na Maendeleo CHADEMA Esther Matiko amesema kuwa endapo wananchi wakimchagua kuwa mbunge ataboresha vyanzo vya mapato vilivyopo.

Matiko aliyasema hayo juzi katika Uzinduzi wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira wa miguu Sabasaba wilayani hapa maarufu Shamba la Bibi.

“Wananchi kama mkinichagua nitahakikisha vyanzo vya mapato vilivyopo vinaboreka sanjari na kubuni vyanzo vipya ili kuongeza mapato nya halmashauri na kuongeza kasi ya maendeleo”alisema Matiko. 

Vyanzo vilivyopo havikudhi haja lakini kuna umuhimu wa kuviboresha sanjari na kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuongeza makusanyo ya mapato ya halmashauri na kuendeleza kasi ya maendeleo.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Demkrasia na maendeleo Chadema wilayani hapa Lukasi Ngoto akimkabidhi Ilani ya chama alisema kuwa hana shaka na Esther kwasbabu ni Mtu wa maendeleo.

“Tunapo amua kufanya mabadiliko hatuna budi kuangalia watu watakaotuletea maendeleo” alisema Mwenyekiti.

Kwa upande wake Mgombea Ubunge jimbo la Tarime wa Chadema John Heche alitoa rai kwa wasimamizi wa uchaguzi hususani mkurugenzi wa halmashauri ya Tarime Athumani Akalama kuwa asijaribu kupindisha matokeo.

Heche aliongeza kuwa Msimamizi wa uchaguzi aache wananchi nwafanye kazi yao na wasiingilie kuvuruga uchaguzi badala yake wafanye kazi waliopewa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa.

Powered by Blogger.