KEMBAKI NITATATUA CHANGAMOTO.
KEMBAKI NITATATUA CHANGAMOTO.
MBOMBEA Ubunge jimbo la Tarime Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi
CCM Michael Kembaki amesema Wananchi wakimchagua kuwa Mbunge atatatua
changamoto zinazowakabili.
Kembaki aliyasema hayo hivi karibuni wakati akihutubia wananchi
waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya
Buhemba shule ya msingi Mazoezi wilayani hapa.
;; Endapo mkinichagua kuwa Mbunge wenu nitahakikisha
ninatatua changamoto na kero za jimbo hili zinazowakabili kama vile
maji,wajasilia mali kuwezeshwa kupata mikopo yenye riba ya garama nafuu ili
kuinua uchumi,pia Elimu na afya zitaborshwa;;alisema Kembaki.
Mgombea huyo alisema kuwa jimbo hilo ni jipya na
atahakikisha Amani inakuwepo kwa lengo la wawekezaji kuja kuwekeza na wananchi
wake hususani vijana kujipatia Ajira.
Aidha kembakai aliongeza kuwa katika sekta ya elimu atzidi
kuboresha kwa lengo la kuwajengea wanafunzi kuazia shule za msingi kupenda
shule.
Naye Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime Vijijini Christopher Kangoye alisema kuwa Magufuri
anauzalendo na nchi yake ni mchapakazi anachukia rushwa nakwamba wakimchagua
hawatajuta kwani wanaotaka mabadiliko hawajawahi kufanya mabadiliko yoyote.
“Uzalendo alionao magufuli utasaidia kiasai kikubwa kuleta
madadiliko endapo wananchi watakuwa tayari kumpa ridhaa ya kuongoza” alisema
Kangoye.
Kwa upande wake Katibu Uchumi wa Chama cha mapinduzi wilaya Tarime
John Gimunta alisema kuwa wananchi waamini chama cha mapinduzi kwa kuwa kina
Ilani na Sera za maendeleo.
‘’Wananchi chagueni CCM Chama cha Amani chenye maendeleo kwa
Wananchi wake ambacho kina sera dhabiti kuliko vyama vingine vya siasa vijana
jua mabadiliko mtayapata ndani ya CCM;;alema Gimunta.
Aidha Gimunta aliongeza kuwa wananchi wakimpa Michael Kembaki
ambaye ni mgombea wa jimbo la Mjini watakuwa wamechagua chaguo sahii
siovinginevyo.