WAZEE NIKICHAGULIWA LAZIMA KUPATA PENSHENI.

Wakwanza kushoto ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la vijana CHADEMA (BAVICHA) Taifa John Heche akiongea na wananchi wa kata ya Nyamwaga kipindi alipokuwa akiomba kura katikati ni Moses Yomami anayewania kiti cha Udiwani kata ya Nyamwaga kupitia Chadema akinadiwa.   

.
WAZEE NIKICHAGULIWA LAZIMA KUPATA PENSHENI.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Bavicha Taifa kupitia CHADEMA John Heche ambaye ni mgombea wa jimbo la Tarime amesema kuwa endapo wananchi wataweza kumpa ridhaa ya kuongoza jimbo hilo atahakikisha wazee kuanzia mika sitini wanalipwa penseni kila mwezi.


Hayo yalisemwa leo  katika viwanja vya soko la Nyamwaga Wilayani Tarime mkoani Mara  kipindi mgombea huyo alipokuwa akiomba kura  kwa wananchi.


John alisema kuwa hilo litawezekana baada ya kuwabana wawekezaji ukiwemo mgodi wa kuchimba dhahabu uliopo Nyamongo wilayani Tarime Mkoani Mara  ACACIA kulipa ipasavyo mapato ya ndni ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na fedha hizo zitapangiwa matumizi ipasavyo ikiwa ni pamoja na kutoa kipaumbele kwa  wazee hao.

"Nina uhakika wajane, wazee kuanzia miaka sitini lazima walipwe penseni baada ya kuchaguliwa kuwa kiongozi wa jimbo hili kwani kila kitu kitawezekena mukisha nipa viongozi wote wa CHADEMA kuanzaia ngazi ya Urais mpka udiwani" alisema John.

Aidha Heche aliongeza kuwa Wananchi wa Mkoa wa Mara wametakiwa kufanya maamuzi yaliyosahihi katika kuchaguza viongozi bora kwa lengo la kunufaika na rasilimali walizopewa na mwenyezi mungu   ikiwemo mbuga ya wanyama Serengeti, Mgodi wa uchimbaji wa dhahabu wa Nyamongo, Mpaka wa Sirari, na Ziwa Victoria kwani kutokana na rasilimali hizo bado wananchi wanakabiliwa na umaskini huku rasilimali hizo zikinufaisha baadhi ya viongozi na wananchi wa kawaida wanazidi kuteseka .

Kwa upande wakeanayewania kiti cha udiwani kata ya Nyamwaga kupitia chadema Moses Masiwa alisema kuwa  serikali imekuwa ikitoza ushuru katika soka la Nyamwaga lakini mpaka sasa soko hilo halina huduma ya choo suala ambalo ni hadha kubwa kwa wananchi hao.

"Wananchi kila soka hapa lazima mutozwe kodi ya mifugo lakini hizo fedha zinakaa Halmashauri kwanini zisirudi kuwasaidia nyie wananchi ukiangalia sheria ya fedha ya serikali zamitaa na vijiji ya mwaka  1982 kifungu cha saba kuwa insema kijiji kinapokuwa na chanzo cha mapato Halmashauri ikiweka mawakala lazima kijiji kilipwe asilimia 25 lakin mpaka tunaongea tangu miaka 50 ya uhuru Nyamwaga hawajawahi kupata asilimia hizo" alisema Moses.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Wilayani Tarime Mkoani Mara Lukas Ngoto alisema kuwa mbali na chama cha mapinduzi kuongoza zaidi ya miaka Hamsini lakini wananchi wanzaidi kukamatiwa kuku na na kubuguziwa huku viongozi wachache wakijilimbikiza mali.
"Udhaifu wa Chma cha Mapinduzi umeonekana kila sehemu hebu nyie wananchi fanyeni maamuzi sahihi kwa lengo la kuleta mabadiliko ya kweli" alisema Ngoto.

Wakina mama nao wamepaza sauti yao kuwa kuwa viongozi watakaochaguliwa waweze kusikiliza kilio chao kwa lengo la kuwainua kiuchumi na kuwapatia ajira
.............Mwisho....


Powered by Blogger.