ACT WAZALENDO, JESHI LAPOLISI SIMAMIA USALAMA BARABARNI.

Anayewania ubunge jimbo la Tarime mjini kupitia ACT Wazalendo Deogratias Meck akiongea na wananchi jana katika mkutano wa hadhara
                                                        Tarime.
ACT WAZALENDO, JESHI LAPOLISI SIMAMIA USALAMA BARABARNI.

Chama cha ACT Wazalendo Wilayani Tarime mkoani Mara kimeomba jeshi la polishi katika kuelekea Uchaguzi kusimamia kikamilifu ulinzi na usalama wa raia ikiwa ni pamoja na kupunguza ajari za barabara huku wakiepukana na kuwabambikiza kesi wananchi kwa sababu ya maslahi ya baadhi ya viongozi suala ambalo linaweza kusababisha migogoro na kuleta machafuko ya Nchi.


Kauli hiyo imetolewana Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo wilayani Tarime Mkoani Mara Paschal Warioba katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana  katika viwanja vya  Serengeti mjini Tarime kwa lengo la  kuwatambulisha viongozi wao ambao wanawania Ubunge, Udiwani na Viti maalumu katika majimbo yote Mawili.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa baadhi ya Askali wamekuwa wakibambikiza kesi kwa wananchi bila sababu za msingi huku wengine wakitumiwa na Viongozi wa vyama mbalimbali kwa maslahi yao binafsi hivyo amekemea suala hilo huku akisisitiza sula la Usalama barabarani.


Mwenyekiti huyo alisema kuwa  katika kata 34 zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na Halmashauri ya Mji wa Tarime  Chama chake kimeweza kusimamisha wagombea  wote ngazi ya Udiwani huku Ubunge jimbo la Mjini akisimamishwa Deogratias Meck na Tarime Vijijni akisimamaishwa Charles Mwera Nyanguru ambaye aliwahi kuwa mbunge wa jimbo Tarime na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.


Hata hivyo Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa Akina mama16 wamejitokeza kugombea viti maalumu katika majimbo yote mawili.


"KWa kuwa chama chetu ni kichanga na ndo tulikuwa tumeanza kujipanga nimehakikisha kata zote zilizopo naweka wagomea  alisema Paschal".

 Kwa upande wake Deogratia Meck ambaye anawania Ubunge  jimbo la Tarime Mjini   kupitia chama cha Act Wazalendo alisema  kuwa  kunahaja ya kuchagua chama chenye sera nzuri ambacho kinatoa kipiaumbele katika sekta ya  ya Elimu kwa lengo la kuondoa Murundikano wa wanafunzi katika shule za msingi huku akiwaasa wafanya bihashara kuwekeza katika Elimu kwa wingi.

Aidha Meck alisema kuwa kawa upande wa wilaya ya Tarime wafanya bihashara wamewekeza sana katika majumba ya starehe na siyo kuwekeza katika suala zima la Elimu hivyo alitumia fursa hiyo kuwashauri wafanya bihashara hao kuwqekeza katika suala zima la Elimu ili kuhakikisha Taifa linakuwa na wasomi wa kutosha kwa lengo la kuondoa utegemezi.

Taifa letu linachangamoto kubwa tunapaswa kuzitekeleza na ajenda za mwaka huu zinapaswa kuwa za kitaalamu ambazo zitaweza kutekelezwa pia jimbo letu nin jipya halina Mgodi na vyanzo vyake vya mapato ni vidogo hivyo hatuna budi kuchaguza viongozi makini watakao weza kuwaletea wananchi Maendeleo alisema Deogrtias.
Powered by Blogger.