WAANDISHI WA HABARI MUSIKUBALI KUTUMIKA.
Picha ya Afisa Programu mwandamizi ubora wa viwango kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT) Alakok Mayombo akifafanua jamabo katika warsha hiyo iliyomalizika hivi karibuni katika jiji la Mwanza. |
WAANDISHI WA HABARI MUSIKUBALI KUTUMIKA.
Mwanza.
Katika harakati za uchaguzi ambao umekuwa ukifanyika hapa nchini na tumekuwa tukiona baadhi ya waandishi wa habari wakibebwa na baadhi ya wagombea na baadhi ya viongozi kwa maslahi yao binafsi
Baadhi ya waandishi wa habari wamekuwa wakitumika vibaya na kukiuka maadili ya uandishi wa habari suala ambalo halitakiwa kwani kitendo hicho kinaweze kusababisha migogoro kwani baadhi ya waandishi wa habari ambao wanakaa na kubeba mikoba ya wagombea wakati wa kampeni hawawezi kuandika habari kwa usawa, kwani watakuwa tayari wamenunuliwa na kuwekwa mifukoni mwa wagombea hao.
Kwa kuliona hilo na hili kuboresha taaluma ya waandishi wa habari Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa kushirikiana na BBC Media Action wametoa fursa ya mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka kanda ya ziwa ikiwemo mikoa ya Mwanza, Geita, Kagera, Mara na Simiyu kwa lengo la kujifunza jinsi ya kuandika habari za uchaguzi hususani tunakoelekea katika chaguzi kuu za october 25 mwaka huu.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa takribani siku tano katika ukumbi wa G &G jijini Mwanza ambapo waandishi wa habari wamehaswa kufuata maadili ya uandishi wa habari kiwa ni pamoja na kuwa na usawa katika kuandika habari hususani za kiuchaguzi.
Aidha waandishi wa habari hao wametakiwa kuandika habari zenye ukweli ndani yake kwa kufuata misingi na weledi wao katika habari kwa lengo la kuepusha migogoro inayoweza kutokea katika harakati za uchaguzi suala ambalo linaweza kusababisha machafuko hapa nchini.
Afisa Programu mwandamizi ubora wa viwango kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT) Alakok Mayombo alisema kuwa Uandishi wa Habari ni Taaluma hivyo wandishi wa habari wanatakiwa kufuata maadili ya taaluma hiyo ili kuifikisha jamii mahali inapotakiwa kufika, na siyo kuandika na kuripoti kile mwanasiasa anataka ufanye kwa kuipotosha jamii.
''waandishi wa habari inatakiwa mripoti habari kwa usahihi, kufuata maadili, ukweli na urari na kusiwe na upendeleo wowote kuepuka kuegemea upande wa chama chochote cha siasa...''
Alisema kuwa tunajua media ina nafasi kubwa sana katika jamii ili wajue wampigie nani na wamwache nani na ataarifa hii hufanywa na mwandishi wa habark ili jamii iwe na taarifa sahihi na mpiga kura awe na taaarifa sahihi juu ya kiongozi yupi amchague na kwa nini amchague kiongozi yule.
Kwa upande wake Mwezeshaji wa Mafunzo hayo Chrysostom Rweyemamu Ambaye ni msahuari wa uhariri na Mafunzo New Habari (2006) Ltd alisema kuwa vyombo vya habari ni mhimili sahihi wenye kuwapa mwanga wapiga kura na jamii kwa ujumla kuhusiana na zoezi zima la uchaguzi.
Alisema kuwa endapo waandishi wa habari na vyombo vyao vikiwa vinaegemea upande mmoja tutakuwa tunawaaminisha wananchi kuwa mgombea yule au chama kile kinafaa zaidi na badala yake tutakuwa tunaipotosha jamii.
''vyombo vya habari vinaweza kubadili mtazamo wa nchi kwa kuegemea upande mmoja wa vyama au mgombea na kuiaminisha jamii mambo yasiyo ya msingi na kukosa ukweli dhidi ya kiongozi yupi bora na yupi hafai''
Aliongeza kuwa waandishi wengi wameanza kukengeuka na kuacha maadili ya taaluma yao kwa kutumiwa na wanasiasa ili waandike na kuuhabarisha umma kile mgombea/chama kinahitaji.
''niwaaombe sana waandishi wa habari tufuate miiko na maadili ya uandishi wa habari ili tuweze kuuhabarisha umma pia tujikite zaidi katika kuandika habari za uchuguzi kuliko za majukwaani''
Naye mshiriki wa warsha hiyo Dotto Bulendu ambaye ni mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Star TV na RFA alisema kuwa vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika kutoa elimu ya uraia kipindi hiki cha uchaguzi, waandishi wanatakiwa kuwajengea uelewa watanzania dhidi ya falsafa na elimu ya uchaguzi na vyama vya siasa Tanzania.
''tujikite zaidi kuchambua mambo kwa kina kuliko kusikiliza sera kwenye majukwaa kwa kuoana mgombea fulani kakusanya watu wengi na tukaacha mambo ya msingi... tuelimishe zaidi wapiga kura dhidi ya vyama vya siasa'' alisema Bulendu.
Mbeki Mbeki ni Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa kagera alisema kuwa asilimia kubwa ya waandishi wa habari wamekuwa wakikiuka maadili ya uandishi wa habari na kwenda kinyume na taratibu na wakati mwingine kubebwa na wagombea jambo ambalo limedhoofisha maadili ya habari huku baadhi ya waandishi wa habari wakisema kuwa asilimia kubwaa waandishi wamejikita sana kuandika habari za kisiasa lakini hakuna anayeandika habari kuhusu fedha zinazoibiwa katika Halmashauri zetu hapa Nchi, Mazingira na Uchumi.
"Halmashauri zetu zimekuwa zikituhumiwa kwa ubadhilifu wa fedha waandishi hatuandiki lakini siasa tumejikita sana kwanini tusibadilike mmoja kati ya waandishi katika kuchagia mada" alisema,
Sambamba na hayo katika uchaguzi mkuu kufanyika October 25 mwaka huu hapa nchini, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetakiwa kuvihusisha vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo Idara ya uhamiaji ili kudhibiti watu wasio Raia wa Tanzania kujiandikisha na kupiga kura.
Hayo yalielezwa hivi karibuni na Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza Remigius Pesambili wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, wanaohudhuria warsha ya uandishi wa habari za uchaguzi inayoratibiwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) na kufadhiliwa na Shirika la Utangazi BBC (Media action Fund) kutoka Mikoa ya kanda ya ziwa.
Alisema kuwa katika zoezi zima la uandikishaji limeonekana kuwa na udhaifu kwa kutowashirikisha idara ya uhamiaji kikamilifu ili kuweza kubaini watu wasio raia wa tanzania kama ilivyovotokea baadhi ya mikoa nchini kukamata wahamiaji haramu wakijiandikisha.
''Katika zoezi la uandikishaji wa kutumia mfumo wa Kieletroniki(BVR) Idara ya uhamiaji haikuhusishwa, Lakini panapotokea tatizo la kubaini wahamiaji haramu idara hii inahusika kushughulikia tatizo moja kwa moja''.
Aliongeza kuwa panapotokea tetesi za mtu kajiandisha na siyo raia wa Tanzania, ndipo tunapopokea kesi na kuanza kizishighulikia lakini hadi sasa zoezi zima linamalizika kwa mkoa wa mwanza hatukuweza kupata malalamiko yeyote wala kesi ya mhamiaji haramu kubainika.
Aliwataka watu waliojiandikisha kupiga kura, endapo watabaini mtu aliyejiandikisha na kuwa si mtanzania basi atoe taarifa idara ya uhamiaji ili waweze kumughulikia.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Hasani Ida alisema kuwa wilaya ya Nyamagana zoezi la uandikishaji wapiga kura lilifanyika kwa amani huku makundi yote maalumu yakipewa kipaumbele.
Alisema kuwa Nyamagana wameandikisha wapiga kura 273,636 sawa na 124% huku wanaume wakiwa 138,523 na wanawake 135,113 wakati huo walitarajia kuandisha wapiga kura 219,636.
''kila aliyejiandikisha siku ya kupiga kura ajitokeze kwenda kupiga kura kuliko kukaa nyumbani na kukosa haki yake ya msingi ya kuchagua kiongozi sahihi''
Aliongeza kuwa tume itahakikisha elimu ya uraia ya kupiga kura ianatolewa kwa tume kuleta vipeperushi, mabango, mashirika mbalimbali, na vyama vya siasa kupewa elimu hiyo.
Hata hivyo taarifa zao kwa sasa zihakikiwa kwenye kata hivyo wajitokeze kwa wingi na wananchi waliojiandikisha kupiga kura wanaweza kuhakiki taarifa zao ka njia ya simu kwa kubonyeza *152*00# na kufuata maelekezo ya tume ya uchaguzi.
Naye mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo alisema kuwa zoezi la uandikishaji wapiga kura limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuandikisha wapiga kura 1,442,391 sawa na 103% ikiwa lengo lao ni kuandikisha wapiga kura 1,403,743.
Hata hivyo Waandishi wa habari pia wametakiwa kuwajibika ipasavyo katika majukumu yao kwa kuwatendea haki wagombea wote pamoja na vyama vyote vya siasa, bila kuegemea upande wowote, ikiwa ni pamoja na kuandika habari za ukweli na kwa usahihi.
Pia waandishi wa habari walitakiwa kuwa makini katika kuandika habari za uchunguzi, ikiwa ni pamoja na kuibua habari ambazo zimejificha ili wananchi waweze kupata ukweli na kuchukuwa maamuzi sahihi ya kuchagua viongozi bora na wanaofaa na siyo bora viongozi huku wakiaswa kuandika habari zinazohusu udanganyifu wa mali za wagombea zilizotamkwa, kuhusu afya zao, elimu yao, kashfa za rushwa, kumbukumbu za wagombea, kashfa katika ofisi za umma, kumbukumbu za polisi, taarifa za awali, uraia wa mgombea na taarifa za awali.
Katika kuandikahabari Kuna changamoto mbalimbali zianzowakumba waandishi wa habari , ikiwa ni pamoja na kusaritiwa na vibaraka waliolipwa, vyanzo vilivyopandikizwa na vinavyotengenezwa, matatizo ya kisheria, kuingilia mambo binafsi, rushwa, kashfa na kushambuliwa kwa kipigo.
Katika mafunzo mkufunzi aliosema kuwa namna ya kukabiliana na changamoto hizo ni kuwa makini na kufuata maadili ya uandishi wa habari na misingi yote ya uandishi wa habari wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.