Wafanya bihashara wajitokeza kumuchukulia Nyambari Fomu ya kuwania jimbo la Tarime Mara ya pili.
Tarime.
Wilayani
Tarime Mkoani Mara wafanyabihashara wa mji mdogo wa Sirari wamejitokeza
kumuchukulia fomu ya kuwania ubunge awamu ya pili aliyekuwa Mbunge wa jimbo la
Tarime Nyambari Nyangwine kwa kile ambacho wamedai kuwa katika uongozi wake wa
miaka mitano ameweza kukomesha vita vya koo kwa koo, kuleta Huduma ya Umeme
pamoja na Baranarakupitika kila mahari suala ambalo limezidi kuwapa imani
wananchi hao.
Wafanya
biashara hao wamedai kuwa kabla ya Mbunge huyo kuongoza jimbo la Tarime
kulikuwepo na vita vya koo na na koo wezi wa mifugo lakini kwa sasa suala hilo
limeisha nawananchi kuishi kwa amani suala amblo wanajinunia kwake ambapo
wameamua kumurudishia fadhila kwa kumuchukulia fomu ili aweze kuwania jilmbo
hilo kwa kutetea kiti chake na hapa wafanya biashara wanaeleza kile
kilichowasukuma kumuchukulia fomu mbunge huyo.
Wakichukua
fomu katika ofisio ya chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ili mbunge huyo aweze
kuwania jimbo la Tarime vijijini huku akitetea kiti chake baada ya majimbo hayo
kugawanywa mara mbili kuwa na jimbo la Tarime Vijijini naMmoja wa wafanya
bihashara hao Mustapha Murimi Marufu kwa jina la Masafa alidai kuwa wameamua kumuchukulia fomu na
kujaza ili waweze kurudisha baada ya kuona utendaji wake mzuri katika kipindi chake ambacho alipewa takribani
miaka mitano.
Kwa Upnde
wake Marwa Mukare alisema kuwa wakati Bunge huyo kipindi anachukua Ubunge
kulikuwepo na Vita vya koo na koo lakini baada ya kuchukua Ubunge suala hilo
limeisha pia ameweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kugawanywa kwa majimbo kwa
lengo la kupanua wigo na kuwaletea wananchi maendeleo kwa ujumla.
“Kabla hajachkua
Ubunge Nyambari kulikuwa na vita baina ya Wairege na na Wanyabasi wanchari na Wakira lakini hayo
yote yameisha na sasa tunaishi kwa amani hiyo tumeamua kumurudisha hawamu ya
pili ili kumalizia baadhi ya vipolo vyake ambavyo vimebaki na kuleta maendeleo”alisema
Marwa.
Kwa sasa
wilayani Tarime Mkoani Mara baada ya Tume ya Uchaguzi kugawanya majimbo nakuwa
na jimbo la Tarime Mjini yenye kata nane na Tarime Vijijini yenye kata 26 hivyo itabidi Wilaya hiyo kuwa na wawakilishi
wawili kwa lengo lakuwaletea wananchi maendeleo.