UWT MUSOMA WAASWA KUSHIKAMANA KUSHINDA UCHAGUZI MKUU.
UWT MUSOMA WAASWA KUSHIKAMANA KUSHINDA UCHAGUZI MKUU.
Musoma
Umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi UWT wilaya ya Musoma mkoa wa Mara, umeaswa kushikamana na kuunganisha nguvu pamoja hatua ambayo imetajwa itakikifanya chama hicho kupata ushindi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi oktober mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa hapo jana na msimamizi wa uchaguzi wa UWT wilaya ya Musoma Mjini Amos Sagara wakati akihitimisha zoezi la uchaguzi wa Madiwani wa viti maalum ndani ya umoja huo, uliofanyika katika ukumbi wa chama cha mapinduzi CCM uliopo mjini Musoma mkoani Mara, ambapo jumla ya madiwani 6 wa viti maalum walichaguliwa watakao ungana na madiwani wa kata ambao watachaguliwa katika uchaguzi mkuu.
Waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni Neima Samson,Zainab Msiba,Amina Shabani,Meleciana Masungura,Rebeka Mkama, pamoja na Rose Magoti ambapo wajumbe walioshiriki katika uchaguzi huo jumla yao walikuwa 300 kutoka katika kata kumi na sita za manispaa ya Musoma, ambapo mara baada ya kuchaguliwa waliombwa kuwa chachu ya hamasa kwa wanawake wengine kukipigania chama hicho ili wakati wa uchaguzi kiweze kurejesha jimbo hilo pamoja na manispaa ambayo ilikuwa ikiongozwa na chama cha Chadema.
Sagara aliwaomba wanawake wa UWT wa wilaya hiyo, kuepuka makundi ambayo yamekuwa yakileta mpusuko hususani nyakati za uchaguzi, na badala yake akawataka kushirikiana bega kwa bega ilikuhakikisha wanafanya vizuri katika uchaguzi mkuu ili kupata viongozi watakao tatua changamoto zinazo wakabili wananchi wa Musoma, ambazo hazikuweza kutatuliwa na serikali ya Chadema ililiyomaliza muda wake ambapo changamoto katika sekta ya Elimu, Afya Miundombinu zikishindwa kupatiwa ufumbuzi yakinifu.
Aliongeza kuwa ili chama hicho kiweze kushinda uchaguzi huo, ni lazima walioshindwa katika uchaguzi huo wa UWT wakubaliane na matokeo na kuwaunga mkono waliochaguliwa badala ya kutengana na kulumbana kwani kwa kufanya hivyo watazidi kutoa mwanya wa kushindwa na hivyo kushindwa kufikia malengo ya kuwapata viongozi watakaotokana na CCM ambao watatoa majibu ya kero za wananchi.
‘’Niwaombe sana wagombea ambao mmeshinda katika uchaguzi huu, shirikianeni kwa pamoja na wenzenu ambao kura hazikutosha kukiimarisha chama iliwakati wa uchaguzi muibuke washindi kwani sri kubwa ya kushinda ni kushikamana na kuweka pembeni tofauti zenu walioshindwa nawaombeni sana nanyi mshirikiane na walioshinda kwani ushindi huu nio wa CCM siyo mtu binafsi’’alisema Sagara.
Awali Kamese Magoti ambae ni Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mara akitoa hotuba yake kwa niaba ya Mgeni rasmi Vedastus Mathayo ambae ni MNEC wilaya ya Musoma mjini, aliwataka wanawake wa umoja huo kuwa makini katika chaguzi zinazofanyika ndani ya chama hicho ilikuwapata viongozi bora watakaopigania maslahi ya wananchi na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kwa ufanisi mzuri sanjari na utawala bora.
Aidha Kamese aliongeza kuwa kwa wale watakaoshindwa katika chaguzi zinazofanyika ndani ya Chama wajifunze kuwa na uvumilivu wa kisiasa badala ya kuhama chama pindi wanaposhindwa kwani kwa kufanya hivyo ni kuonesha ukomavu wa Demokrasia ndani ya CCM tofauti na vyama vingine vya upinzania hapa nchini.