DC KANGOYE ATANGAZA NIA KUWANIA JIMBO LA TARIME VIJIJINI,

Picha ya DC kangoye amevaa njano aliyetangaza nia ya kuwania jimbo la Tarime Vijijini CCM akiongea na waandishi wa habari kuhusu vipaumbele vyake



DC KANGOYE ATANGAZA NIA KUWANIA JIMBO LA TARIME VIJIJINI,
MKUU wa Wilaya ya Arusha Christopher Kangoye anayetangazania ya kugombeaUbunge Jimbola TarimeVijijini  kupitia CCM,amesema kuwa hajakata tamaa kutangazania licha yakuwa ni mara yake ya nne kutangaza nia ambapo alishatangaza mara tatu na akaangushwa kwenyekura za maoni za CCM.

Akizungumza na waandishi wa Habari  Wilayani Tarime Kangoye alisema kuwa ni mara yake ya nne kutangazania na hii inaonyesha  ni kwakiasi gani anawapenda wananchi wa Tarime nakwamba hajakata tamaa licha yakuwa yeye ni Mkuu wa Wilaya.

Kangoye alisema kuwa ametangazania baada ya kujitathmini uzoefu alionao Serikalini tangu alipokuwa Mfanyakazi Mamlakaya mapato Tanzania(TRA) nakisha kuchaguliwa na Rais Kikwete Kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kwimba-Mwanza,Mpwapwa-Dododma na Arusha.

“Nitatumia uzoefu wangu nimefanya kazi Serikalini za kutumikia wananchi mimi ni Mkuu wa Wilaya wananchi wananifahamu  ni mashahidi hata ninapohamishwa husikitika nahitaji Tarime iwe ya maendeleo nitatenda haki maana bila haki hakuna amani na bila amani hakuna maendeleo wananchi wanatarajia changamoto zitatuliwe”alisema Kangoye.

Mtangazania huyo alisema kuwa sababu ya kugombea anapenda awatumikie wananchi wa Tarime awe mwakilishi wa wananchi ikiwa nipamoja na kuchukuwa mawazo yao kuyafikisha Seriklini kama kutimiza majukumu ya ubunge na kuisimamia Serikali kutekeleza mahitaji ya wananchi.
Aidha kangoye alisema kuwa endapo ataweza kupitishwa na chama chake atahaikisha anawatumikia wananchi wake ikiwa ni pamoja na kutekeleza ilani ya chama chake kwa lengo la kuhaminisha wananchi na kuzidi kukiamini chama cha mapinduzi ikiwa ni pampja na kupanua wigo wa ajira kwa vijaba kupitia utalii wa ndani.
"Hapa kwetu tuna migodi pamoja na hifadhi lakini vijana wetu hawana ajira nikisha pata fursa hiyo lazima niweke mikakati ili vijana waweze kupata ajira" alisema kangoye.

Selemani Moya ambaye ni Diwani wa Kata ya Kibasuka Kupitia CCM alisema kuwa Dc Kangoye anafaa kuwa Mbunge kwakuwa ni mtu asiye na makundi,fitina lakini anaonekana ana nia ya kutumikia wananchi na dhiyo maana anapoanguka kura za  maoni haonyeshi kukata tamaa.

Marwa Mwita mkazi wa Tarime mjini alisema kuwa Huwenda Kiongozi huyo asipite kura za maoni kwani chama cha CCM kimekuwa kikimbeba mtu ambaye anawawezesha kifedha hivyo huwenda amuombe Mungu amfungulie njia kwani shida ipo kweny chama chake na si kwa wananchi.
Powered by Blogger.