KEMBEKI ATOA VIPAUMBELE SEKTA YA ELIMU NA MAJI.
Picha ya Michael Kembaki akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani jana kuhusu vipaumbele vyake endpo atafanikisha kupeperusha bendera ya chama cha mapinduzi CCM Jimbo la Tarime Mjini. |
KEMBEKI ATOA VIPAUMBELE SEKTA YA ELIMU NA MAJI.
Mkurugenzi mtendaji wa Memolia Foundation iliypo jijini Arusha Michael Kembaki ambaye yuko kwenye kinyanganyiro cha kuwania Ubunge jimbo la Tarime Mjini kati ya Watia nia sita waliojitokeza amesema kuwa yeye vipaumbele vyake vya kwanza ni pamoja na Elimu na Maji kwani vitu hivyo ni muhimu sana kwa mahitaji ya mwanadamu
Akiongea na waandishi wa habari katika Hotel ya Goldland Wilayani Tarime Mkoani Mara Kembaki amesema kuwa amekuwa mstari wa mbele katika kutoa msaada kwa watu wenye mahitaji maalumu , Wajane Vikundi vya kuweka na kukopa SACCOS kwa lengo la kusukuma gurudumu la maendeleo ikiwa ni pamoja na kuendeleza wilaya Ya Tarime.
Aidha kembaki ameongeza kuwa ameamua kuwania kiti cha ubunge Jimbo la Tarime mjini kwa lengo lakuwakilisha wananchi wa Tarime na Mkoamzima wa Mara bila kusahau watanzania wote bila ubaguzi wowote wa dini wala kabila ili kuweza kusukuma gurudumu la Maendeleo.
Hata hivyo Kembaki amedai kuwa endapo atafanikiwa kupitishwa na chama chake na kuweza kupeperusha bendera ya Chama hicho ataweza kutoa vipaumbele katika sekta ya Elimu pamoja na Maji, huku akiboresha michezo lika zote kwa lengo la kuwaandalia vijana ajira za moja kwa mojakupitia michezo na vikundi hivyo vya ujasiliamali.
Amesema kuwa katika sekta ya Elimu kuna upungufu mkubwa wa Madawati , Upungufu wa Madarasa suala ambalo linapelekea wanafunzi kurundikana darasani ni chanzo hichokinaweza kuchangia kushkuka kwa taaluma,pia suala hilo katika maeneo ya Mjini inachangia wanafunzi kusoma kwa hawamu huku wengine wakiingia mchana na wengine asubuhi sula ambalo linachangia utoro kwa wanafunzi hao.
Pia suala zima la ukosefu wa Maji ni tatizo kubwa katika maeneo ya mjini huku wananchi wanatumia visima vya asili ambavyo siyo salama kwa afya zao, hivyo kupitia serikali kama ataweza kupewa ridhaa ya kuongoza amedai kuwakuboresha maji ya visima kwani jamii bado wanatumia visima vya asili ambavyo siyo salama kwa afya yao alisema Kembaki.
Katika jimbo la Tarime Mjini wanaowania kiti cha ubunge kupitia Chama cha mapinduzi ni pamoja na Waziri wa kazi na Ajira Gaudensia Kabaka,Michael Kembaki,Philipo Nyirabu, Jonathani Machango,Ditu Manko na Brito Burure.