Mwenyekiti wa baraza la vijana Chadema asema yeye ni Tumaini jipya kwa wanatarime.
Picha ya mwenyekiti wa Baraza la vijana BAVICHA Chadema Wilayani Tarime Mosses Yomani akiongea na Mmiliki wa Blog hii kuhusiana na mustakabali wa kuwania jimbo la Tarime Mkoani Mara.
Tarime.
Mwenyekiti wa baraza la vijana Chadema asema
yeye ni Tumaini jipya kwa wanatarime.
Mwenyekiti wa Baraza la vijana
Chadema Wilayni Tarime Mkoani Mara (BAVICHA) Moses Yomami ambaye pia ni
mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na maendeleo chadema Kanda ya Serengeti
ambayo inajumuisha Mkoa wa Mara, Shinyanga na Simiyu amesema kuwa ameamua kutia
nia ya kuwania jimbo la Tarime baada ya kuona rasilimali zilizopo katika mkoa
wa Mara kutonufaisha wananchi baada ya viongozi ambao wamekuwa wakichaguliwa
kutotumia vizuri vipaumbele vilivyopo.
Katika harakati za kutangaza nia kwa lengo la kuwania jimbo la Tarime Mkoani
Mara Bw :Moses misiwa yomami ni moja kati ya watiania hao huku akibainisha
vipaumbele vyake na suala ambalo limemusukuma kuwania kiti hichi cha ubunge.
Moses alisema kuwa
yeye ni kijana ambaye ni tumaini jipya katika jimbo la Tarime hivyo
wananchi hawana budi kufanya maamuzi yaliyosahii katika kumuchagua pale
atakapopendekezwa na chama chake ili kuweza kupeperusha bendela ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kwa lengo la kusukuma gurudumu la maendeleo kwa
kushirikisha wananchi wotena rasilimali zao.
Akiongea na gazeti hili Mtia nia huyo alitoa historia yake
kuwa Bw moses aliyezaliwa kijijini
nyamwaga mwaka 1987 wilayani Tarime ana
shahada ya sheria kutoka chuo kikuu cha mtakatifu agustine jijini mwanza na kwa
sasa ni miongoni mwa wanasheria wa chama hicho katika kanda ya Serengeti.
Kiongozi huyo aliongeza kuwa kutokana na wilaya hiyo kuwa na ardhi nzuri na mvua za
mara kwa mara kipindi cha masika ikiwa ni pamoja na kuwa na madini mengi lakini
bado rasilimali hizo hazimnufaishi mwanachi wa kawaida kwa kiasi cha kuridhisha
ameamua kuwania kiti hicho ili akiweza kupata fursa aweze kuzitetea kwa lengo
la kuwaletea wananchi maendeleo.
“Changamoto za
elimu,upungufu wa walimu,vifaa vya kufundishia
mashuleni,usimamizi mbovu wa mapato ya halmashauri ulipaji mbovu wa kodi
kwenye makapuni ya uwekezaji tuliyonayo,sekta ya afya ni aibu madawa
hamna,uhaba wa manesi,madaktari na majengo
mabovu,sekta ya kilimo na mifugo hatuna ofisi za watalamu wa kilimo na
mifugo ingawaje tunasikia kuna vyuo vikuu vya kilimo kama sua lakini bado
wananchi wanakufa na umskini” alisema Mwenyekiti.
Anabainisha kwamba wilaya ya Tarime inalima mazao ya chakula
na biashara ambayo yana soko katika upande mwingine wa Afrika mashariki hasa
nchini Kenya lakini ni vigumu kwa
wananchi kusafirisha mazao hayo kutokana na vizuizi vilivyowekwa.
Hivyo alisema kuwa atatumia
jukwaa la majadiliano kwa lengo la kuona mwananchi ananufaika na rasilimali inayomzunguka ikiwa
ni pamoja ya kupigania utetezi katika kuwepo kwa mikataba yenye tija kwa
mwananchi kupitia makampuni ya uchimbaji
madini.
Moses yomami anasema akiwa kiongozi wa wanafunzi wa vyuo
vikuu kutoka vijiji vinavyozunguka mgodi wa acacia uliopo Nyamongo Wilayanio
Tarime Mkoani Mara waliokuwa wakisomeshwa na kampuni hiyo,amebaini kumekuwepo
mabadiliko ya majina ya kampuni hiyo ya madini huku wakurugenzi wake wakiwa ni
walewale kitendo kinachoashiria kuwepo kwa udanganyifu katika ulipaji wa mapato
serikalini anabainisha pia kuwa akiwa bungeni atashawishi bunge kwa hoja
binafsi kubadili mfumo wa sheria za kodi na misamaha ya kodi kampuni za
madini zinalipa asilimia 0 kwenye bidhaa
zinazotoka nje ya nchi lakini za uchimbaji wakati wa utafiti mpaka mwisho na
mpaka mwishoni mwa mwaka wa kwanza wa uzalishaji na baada ya hapo wanalipa 5%
kampuni hizi pia zinalipa asilimia 0%
kama kodi ya mafuta wanayoagiza nje.
Aliongeza kuwa pamoja na mgodi huo wa acacia kusomeshwa
vijana kwa elimu ya chuo kikuu,atanzisha mjadala na kampuni hiyo iweze
kusomesha wanafunzi wote wa sekondari kama ambavyo tumejadili wameanza kijijini
nyamwaga kulipia wanafunzi hao kwani kilakitu kinawezekana ukiweka mkakati
safi.
………Mwisho….