Shirikisho la vyama vya tiba asili Tanzania Watoa tamko Mkoani Mara.



                                             Musoma
Shirikisho la vyama vya tiba asili Tanzania Watoa tamko Mkoani Mara.
Shirikisho la vyama vya Tiba asili Tanzania( SHIVYATIATA) wametoa tamko juu ya utendaji wake wa kazi baa da y a mwenyekiti  wa shirikisho  la vyama hivyo TanzaniaBw: Abdulrahaman Mussa Lutenga  kutoa tamko la awali kwa taifakuhusu sheria inayolinda na kusimamia vyama hivyo huku wakikemea baadhi ya waganga wanaofanya kzi zao bila kuwa na kibali huku wakitumia nyara za serikali kuwa hawana budi kutambua umuhimu wa shirikisho la vyama vya Tiba asili.

Akiongea na waandishi wa habari Mwenyekiti wa shirikisho hilo ngazi ya Mkoa Jacobosira Matiko alisema kuwa katikakuboresha na kuendeleza huduma ya tibaasili hapa nchini na mikoani serikali militunga sheria na23 ya mwaka2002 ya tiba asili na tiba badala ili kuhakikisha azima hiyo ya wizara ya Afya na ustawi wa jamii,ilikaa na vyama vyatiba asili na kuvishauri kukaa pamoja na kuunda chombo kimoja kitakachokuwa kianafanya kazi na serikali kutokana na ushauri huo vyama hivyo viliweza kukubaliana na kuunda shirikisho la vyama vya tiba asili Tanzania yaani Shivyatiata na mchakato huo ulianza 2003 kwa lengo la kufuta sheria na kanuni za nchi.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa malengo ya vyama hivyo ni kuwa wanaleta ushiriukiano wa kutosha kwa kushirikiana na Serikali, mashirika ya kitaifa na kimataifa, kuratibu na kusimamia  na kutoa taarifa za tiba asili kudhibiti na kutetea taaluma za tiba asili huku wakizidi kuahamasisha waganga wanajisajili nakuweza kutambulika serikalini ili kuepuka changamoto ambazo zimekuwa zikiwasakama ikiwa ni pamoja na serikali kuwasakama wale wasiotambulika.
Aidha Matiko alisema kuwa Mkoa wa Mara  inakadiliwa kuwa na tiba asili wasiopungua 2000 kati ya wanatiba75 elfu waliopo hapa nchini na ili watu hao wawezekufanya kazi kwa mujibu washeria ni lazioma waweze kusajiliwa  na kufuata taratibu na kanuni za Nchi.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema kuwa kumekuwepo changamoto za uharifu kupitia mwamvuli wa Tiba asili kutokana na wagagnga wanaohama kutoka mkoa mwingine kwenda mkoa mwingine na waganga hao usafiri bila kufuata taratibu na kanuni  hivyo amesem akuwa hawanabudi kutambua mwongozo na sheria ya tiba asili ya mwaka 2002 kufuatwa ili kupunguza chanagamoto zinazowakabili.

Aidha Jacobo sira aliongeza kuwa Machi 9 mwaka huuShirikisho la tiba asili liliweza kutoa tamko kupoitiavyombo vya habari kuungana na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Bunge la Jamhuri viongozi wa dini na vyama vya siasa kutokana na vitendo vinavyoendelea kutendeka  kuhusu mahuaji ya binadamu wenye ulemavu wa ngozi  pamoja na vikongwe  ambapo chanzo kilikuwa ni waganaga hao  hivyo uongozi wa shirikisho hilo ngazi ya mkoa waliweza kuweka mikakati31 ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ili jamii kuondokana na imani potofu.

Mwisho alisisitiza kuwa Mganag yeyote au mkunga ambaye anamiliki Nyara za serikali ambazo zinatumika katika  kufanyia kazi anapaswa kuwa na barua kwa ajili ya kulinda usalama wake pale anakamatwa na jeshi la polisi
…..MWISHO…
Powered by Blogger.