Aliyejifungua mapacha watatu Tarime aomba msaada kwa serikali.

Picha ya Baba mzazi na mama mzazi waliosimama nyuma ya diwani wa kata ya Matongo Nyamongo wakiwa wamebeba watoto hao
Aliyejifungua mapacha watatu Tarime aomba msaada kwa serikali.
Wilayani Tarime Mkoani Mara Mama mmojaanayejulikana kwa jina la Suzana Limo mwenye Umri wa miaka 23 mkazi wa kijiji cha Ngerengere kata ya Nyamaraga  Tarafa ya Inchugu  Wilayani hapa ameiomba serikali kumpa msaada ili kuweza kulea watoto wake ambao amejaliwa na mwenyezi mungu.
Suzana alisema kuwa baada ya kujifungua watoto hao ambao kwa sasa wako na miezi Saba lakini bado Afya zao zinzendelea kuwa dhaifu kwa sababu ya ukosefu wa lishe bora hivyo ameiomba serikali na Taasisi zisikuwa za kiserikali yakiwemo mashirika mbalimbali kutoa  msaada kwa lengo la kuokoa maisha ya watoto hao ambao mpaka sasa wako hai japokuwa afya zao ndo dhaifu kwa kukosa mahitaji muhimu.
“Mimi baada ya kujaliwa watoto hao maisha yangu ni magumu nimekuwa nikilala kwa kutandika Magunia nalala njaa watoto wanakunywa chai isiyokuwa na sukari wakati mahitaji yao ni maziwa kwa ajili ya lishe lakini mimi na mme wangu maisha yetu ni magumu zaidi” alisema Suzana.
Limo Maremo 44 ni baba mzazi wa watoto hao alisema kuwa mtoto wa kwanza ni wakike anajulikana kwa jina la Grace Limo wapili ni msichana Greshezi Limo na watatu ni mvulana anayetambulika kwa jina la Derick Limmo alisema kuwa watoto hao mpaka sasa wako na miezi saba lakini hawazidi uzito wa kilo mbili na Mwingine mmoja kilo 3 suala ambalo limemuangaisha sana katika kuomba msaada ili kuweza kukidhi mahitaji ya watoto hao.
“Huyu mke wangu ni Mke wa pili kwangu hivyo bado familia mbili zinanitegemea ninashida nyingi nanilikuwa na mifugo yangu iliibiwa yote hivyo kwa sasa sina lolote” alisema Baba mzazi huyo.
Katika kuunga juhudi hizo na kutoa msaada baada ya jamii nzima kuguswa na suala hilo Mbunge wa viti maalumu CHADEMA Mkoa wa Mara Esther Matiko ametoa  godoro moja kwa ajili ya kulalia,   pia ametoa bili ya maziwa mpaka watoto hao watakapofikisha mwaka mmoja, Vyakula vya lishe kama vile Ulezi, Karanga ,Mchele ili viweze kusagwa kwa pamoja na kuwapatia watoto hao ili waweze kuwa na afya ya kutosha ili kuokoa maisha yao.
“Mimi ni Mbunge poa ni Mazazi hivyo ni wajibu wangu kusaidia watu wenye mahitaji kwa lengo la kunusuru maisha yao na kuwaondolea msongo wa  mawazo pia ni wananchi wangu ambao pia nawatumikia”alisema Matiko.
Kwa upande wake Diwani wa viti maalumu kata ya Matongo Nyamongo Philomena Tontora alisema kuwa mama huyo kama atakuwa tayari ataweza kumuifadhi kipindi cha Mwezi mmoja nyumbani kwake ili kuweza kuwasaidia watoto hao kwani wanahali mbaya sana huju Afisa Tarfa Ya Inchage Wilayani hapa Upendo Kaswaga  akitoa Balanketi 4 za watoto,Neti  3 za watoto , kofia 2 na Masewta Mawili ili watoto hao waweze kijisitili.
Hata hivyo mama huyo aliweza kufika mbele ya Kikao cha kuvunja  baraza la madiwanii katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na madiwani hao waliweza kumuchangia mama huyo ili kuweza kunusuru maisha ya watoto hao suala ambalo limeweza kurudisha faraja kati ya Wazazi hao wote wawili.
………….Mwisho…



Powered by Blogger.