Mgombea Udiwani kata ya Nyanungu atoa vipaumbele kwa vijana.
Katibu wa Chama cha mapinduzi kata ya Nyanungu akikabidhi fomu kwa mgombea wa udiwani kata ya Nyanungu Marwa Daud Ngicho hap jana |
Tarime.
Mgombea Udiwani kata ya Nyanungu atoa
vipaumbele kwwa vijana.
Mmilikiwa
Mgodi wa wachimbaji wadogo Mosege uliopo nyamongo wilayani Tarime Mkoani Mara
Marwa Daudi Ngincho ambaye kwa sasa ameingia katika ulingo wa siasa kwa lengo
la kuwaletea wananchi wake maendeleo baada ya kuona uongozi uliopo ndani ya
kata kutotenda haki kwa wananchi wake
ikiwa ni pamoja na ukosefu wa huduma ya Afya, Maji na Elimu,
Akichukua
Fomu ya kuwania Udiwani kata ya Nyangungu Ngicho alisema kuwa ameamua kuwania
kiti hicho kwa lengo la kupata nafasi hiyo ili kuendelea kusaidia vijana Akina
Mama na wzee ili kila mtu aweze kuwa na maisha mazuri na siyo tegemezi kwa kila
kitu.
Alisema kuwa
kabla ya kuwa kiongozi kupitia mgodi wake wa wachimbaji wadogo uliopo Mosege
ameweza kutoa ajilia kwa vija zaidi ya 420 ambao pia walikuwa wakijiusisha na
suala zima la uwindaji haramu katika Hifadhi ya Mbuga ya wanya Serengeti.
Aidha daud
aliongeza kuwa ameweza kufungua vikindi nane vya akina mama na kuviwezesha pesa
ili viweze kujiendesha lengo kubwa ni kubadili maisha ya wakazi wa kata ya
Nyanungu.
“Uongozi
ambao tulichagua katika kipind kinachomalizika ulikuwa ni CHADEMA alakini hawakuweza kuwatetea wananchi
sasa lazima wananchi wafanye mahamuzi yaliyo sahihi ili kuleta kiongozi aliyebora” alisema Ngicho.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa kata ya Nyanungu Damian Munge aliongeza kuwaKatika kuleta na
kudumisha amani hapa Nchini kwenye
mchakato ulipo mbeleni wa uchaguzi wa Madiwani Wabunge na amewaomba viongozi mbalimbli wakiwemo viongozi
wa kiserikali kusimamia haki katika uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na kuondokana
na siasa zenye maji taka kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.
Kauli hiyi
imetolewa na mwenyekiti huo katika ofisi ya chama kata kipindi Kipindi cha mgombea huo anaye wania kiti cha
udiwani kupitia CCM kata ya Nyanungwa Marwa Daud Ngicho alipokuwa akichukua fomu ofisini hapo.